Search This Blog

Saturday, June 11, 2011

WACHEZAJI WA KIINGEREZA WANAPENDA SANA STAREHE


ROBIN VAN PERSIE amewaponda wachezaji wa kiingereza kuwa wanapenda sana starehe kuliko kucheza soka.

Van Persie anasema anashangazwa sana na tabia za baadhi ya wachezaji hao, "Ninapoona baadhi ya wachezaji wa kiingereza wanakesha nje mpaka saa 9 usiku huwa napata jibu moja tu kuwa watakuwa hawana thamani watakapofikisha umri wa miaka 33.Kwangu mimi ni muhimu sana kuwa napata kifungua kinywa na wanangu wawili asubuhi,na hiyo haitawezekana kama utakuwa unahangaika kwenye madisko usiku mzima.Nikifanya uamuzi mwingine basi itakuwa ni kufanya kitu ninachokipenda kucheza soka." alimaliza Van Persie.


No comments:

Post a Comment