Search This Blog

Wednesday, June 29, 2011

UBAVU WA KUSHOTO WA KIPA MPYA WA MAN UNITED

Ulimwengu mzima una taarifa za Manchester United kumsajili kipa kinda David De Gea kama mrithi wa Edwin Van Der Saar . Kuna jambo moja ambalo limewapita nalo ni rafiki wa kike au mpenzi wa De Gea . Kama inavyotambulika kuwa marafiki wa kike , wapenzi na wake wa wacheza soka ni ‘hot cake’ nchini England na hakika mpenzi wa De Gea anaingia moja kwa moja kwenye mkumbo huo . Binti mwenye umri wa miaka 25 Edurne ndiye mpenzi wa De Gea na hajaupata umaarufu kwa ajili ya De Gea kwani na yeye ni maarufu kwa upande wake kutokana na kazi anayoifanya ambayo ni uimbaji . Tazama clip ya video yenye wimbo wake hapo chini na ndio utakapotambua kuwa De Gea anakuja Old Trafford si tu kuchukua namba iliyoachwa wazi na Edwin Van Der golini bali amekuja kuchukua ufalme uliochwa wazi na David Beckham na malkia wake posh spice .­
http://www.youtube.com/v/wD3FY2fOd7Q?version=3&hl=en_US">

No comments:

Post a Comment