Search This Blog

Monday, June 6, 2011

TURKISH FA - HIDDINK AMEFUNDISHA MECHI YAKE YA MWISHO JANA


Guus Hiddink yupo njani kuelekea Stamford Bridge baada ya shirikisho la soka la Uturuki kusema kuwa "amefundisha mechi yake ya mwisho".

The Dutchman amekuwa anatajwa kama ndio mrith sahihi wa Carlo Ancelloti aliyefukuzwa baada ya ligi kuu kuisha, na sasa inaonekana Hiddink mwenye umri wa miaka 64 anataka kurudi darajani kwa mujibu mabosi wa FA ya Uturuki .

A TFF source ameiambia BBC kuwa "Hiddink hawezi kusema hapana kwa Chelsea, na tunaamini anataka kuondoka."

Aliongeza: "Hiddink anasema ana mkataba lakini hizi ahadi hazina maisha, Chelsea wanatoa ofa nzuri vigumu kuikataa na shirikisho linaelewa hili suala.Hiddink anajisikia bado ana kazi ya kufanya pale,anataka kwenda pale na ligi na labda baadae Champions League. FA tunaamini kwamba Guus amefundisha mchezo wake wa mwisho jana ikiwa Chelsea italipa fidia ya kuvunja mkataba wake".

The former Holland and Real Madrid boss alishinda kombe la FA alipokuwa na Chelsea mwaka 2009 akiwa kocha wa muda wa timu hiyo.


No comments:

Post a Comment