Search This Blog

Friday, June 10, 2011

TFF YAKANUSHA KULA PESA ZA ZAWADI ZA WASHINDI WA LIGI KUU YA VODACOM

Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF limekanusha taarifa za kwamba , TFF imetafuna fedha za ubingwa wa Tanzania Bara zinazotakiwa kupewa mabingwa wapya Dar es salaam Young Africans.

Akikanusha taarifa hizo katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema kwamba TFF walifanya makubaliano na Uongozi wa klabu ya Yanga juu ya namna ya kupewa fedha hizo na hadi sasa tayari wameshamaliza kulipa kiasi cha fedha walizokuwa wanadaiwa na club ya Yanga. Pia amekiri kutokulipwa kwa muamuzi bora ,na cheki ya mchezaji bora amesaini hivi karibuni .

No comments:

Post a Comment