Search This Blog

Friday, June 10, 2011

KING ERIC KUREJEA OLD TRAFFORD


ERIC CANTONA atarudi Theatre Of Dream mwezi August kwa ajili ya kucheza mechi ya kumuaga Paul Scholes.

Scholes ambaye alitundika daluga mwishoni mwa msimu uliopita, anategemea kuagwa na mashabiki wengi katika mechi dhidi ya New York Cosmos.

Uwepo wa Cantona kama kocha unaonekana utazidi kuongeza mahitaji ya tiketi.

King Eric mwenye umri wa miaka 45 alisema: "Nataka kumpongeza Paul kwa kuwa na na kipindi kizuri na Unite, naangalia mbele kurudi OT katika jukumu langu kama kocha wa New York Cosmos.Huu utakuwa usiku mkubwa kwangu na familia yangu hivyo najipanga kufurahia kila kitu siku hiyo."


No comments:

Post a Comment