HARRY REDKNAPP amewaambia Man United watakuwa wanaota kama wanadhani atamuuza Modric kwa paundi million 20.
United manager Alex Ferguson ni shabiki mkubwa wa Modric lakini Redknapp anasema hana mipango ya kumuuza Luka wala Gareth Bale.
"Nimekuwa nikisikia mazungumzo kuhusu paundi millioni 20 kwa ajili ya Luka, watakuwa wanaota kuwa nitakubali kumuuza mchezaji mzuri kama Modric kwa pesa hiyo.Tottenham sasa tunajenga timu na sio kuibomoa kwahiyo hatuna mpango wa kuwauza Luka au Bale, itakuwa hatua kubwa sana kurudi nyuma ikiwa tutawauza hasa kwa bei ndogo kama hiyo". - Redknapp.
No comments:
Post a Comment