Search This Blog

Friday, June 17, 2011

NI MUDA WA FABREGAS KUONDOKA ARSENAL


Muda umefika kwa Arsenal Wenger kuwa na maamuzi sahihi kwa kuamua kufanya maamuzi ya kijasiri ya kumuuza Cesc Fabregas.
Naamini kila ambavyo Fabregas anapolilia kurudi Catulunya ndivyo ambavyo uwezo wa kuisadia Arsenal utakavyopungua, kama mchezaji na kiongozi uwanjani.
Ni wazi kabisa kuwa Fabregas anataka kujiunga na timu ambayo imemlea na kumkuza kama mchezaji, hata amejaribu kudhihirisha mapenzi yake kwa Barca kwa kuamua kuchora tattoo ya motto wa Barca 'Mes que un club'.
Fabregas amejaribu kutimiza ndoto yake kuwa kweli katika kipindi cha misimu 3 iliyopita na bado Wenger mara zote amekuwa akisisitiza mchezaji huyo hauzwi.
KWANINI TUWE TUNASIKIA HUU UJINGA KILA UNAPOFIKA WAKATI WA USAJILI

Cesc anazidi kuchanganyikiwa na kukosa umakini katika kuitumikia Arsenal.Wenger alimpa kitambaa cha unaodha Fabregas kuonyesha ni kiasi gani anamuhitaji mchezaji na anapenda aendelee kubaki Emirates na sio kwa sababu Cesc angeweza kuwa kiongozi mzuri.
Ikiwa unajua timu inaongozwa na mchezaji ambaye anapenda kwenda kucheza timu nyingine basi huyo sio kiongozi katika kuwahamasisha wenzie kuipigania timu kwa mapenzi yote.

Fabregas akiwa majeruhi hakujishughulisha hata kidogo kwenda kuiangalia na kuhamasisha wachezaji wa timu anayoiongoza ikicheza mechi ya mwisho ya ligi dhidi ya Fulha, mchezo ambayo kimsingi ilikuwa ni muhimu kwa timu katika kujihakikishia nafasi ya kucheza Champions League, badala yake bwana mkubwa Fabregas aliamua kwenda kuangalia mashindano ya mbio za magari "Spanish Grand Prix".Inaonekana Fabregas hakuwa anajali kama ambavyo nahodha wa Liverpool Steven Gerrard ambaye pamoja na kuwa timu yake alikuwa imeshakosa nafasi ya kucheza Champions League alienda kuangalia timu yake akicheza dhidi ya Aston Villa.
.
Fabregas aliulizwa wiki hii kuhusu sakata la Samir Nasri kama mfaransa huyo anapaswa kubaki au kuondoka Emirates alisema: "Samir ana furaha hapa lakini sijui ni kitu gani bora kwa ajili yake".Hii ina maana Fabregas anakosa uhalali wa kumwambia Nasri asiondoke wakati yeye mwenyewe(Fabregas) nataka kuihama klabu hiyo.
Hivi juzi Bacary Sagna amesema ni bora Fabregas aondoke: "Cesc anahitaji kurudi kwenye nchi yake, nyumbani kwake, kuungana na familia yake.Anahitaji kucheza katika moja ya vilabu bora duniani ambayo ni Barcelona."

Mashabiki wengi wa Arsenal wanatofautiana kuhusu Fabregas ambaye msimu uliopita hakuwa katika kiwango kizuri na hakuwa timamu kiafya.
Naamini mashabiki watakubaliana na kuuzwa kwa Fabregas akiwa Wenger atatumia pesa na kusajili wachezaji bora,ikizingatiwa ni ukweli kwamba Arsenal haijashinda kombe lolote tangu Fabregas aje ukiacha kombe la FA ambalo walichukua miaka 6 iliyopita.

Sir Alex Ferguson alijua muda sahihi wa kumuuza Cristiano Ronaldo, United hawakuwa na furaha kuwa na kikosi bila Ronaldo na Ferguson kama angeweza angemrudisha mvhezaji huyo hata leo lakini Boss huyo wa Man United anajua kuuzwa kwa Cristiano ulikuwa ni uamuzi chanya kwa kuwa mchezaji alishaonyesha nia ya kutaka kuondoka hivyo kuendelea kumn'ganinia kungeshusha hadhi ya timu.
Wenger anahitaji kuchukua falsafa ya Fergie kuwa hakuna mcheza mkubwa kuliko timu kwa kuamua kumuuza Fabregas na kutumia fedha kushindana kusajili wachezaji bora duniani.
Kuendelea kumng'aninia Fabregas sio uimara bali ni udhaifu na inaonyesha kuwa Wenger hajui ni jinsi gani ataenwesha timu bila mhispania huyo.

Naamini Arsenal imewahi kuwa na wachezaji bora kuliko Fabregas, tuikumbe Gunners ya akina Tony Adams na kizazi bora kabisa ambacho kiliweka historia nzuri katika ulimwengu soka duniani, hakikuwa na Cesc lakini kilipata mafanikio makubwa.Hivyo kuondoka kwa Fabregas kunaweza kumaanisha kuzaliwa upya kwa Arsenal ambayo italeta furaha iliyopotea katika sura za mashabiki wa GUNNERS.

Naomba kuwasilisha.


No comments:

Post a Comment