Search This Blog

Thursday, June 16, 2011

MUDA WA KUHAMIA ENGLAND UMEWADIA: SAMUEL ETO'O


Samuel Eto'o ametoa habari za kuwashtua wapenzi na mashabiki wa Inter Milan baada ya kusema anatamani kujiunga na ligi kuu ya England- Premier Lague.

Ujumbe huu wa Cameroon straiker umekuja masaa 24 baada ya Inter kuthibitisha kuwa kocha wao Leonardo yupo mbioni kujiunga na PSG.
Eto'o ameliambia gazeti la Corriere dello Sport:
"Nafikiria kuhusu kuhusu suala hili, nina mwezi mzima wa kuamua juu ya hili ama niondoke au nibaki.Nina umri wa miaka 30 sasa hivyo inabidi nifikirie vizuri kabla sijasaini mkataba mpya. Niliamua vizuri kucheza Italy na sasa akili yangu inaniambia muda wa kucheza England umewadia."


Kauli ya Eto'o inategemea kuzusha mapigano makubwa miongoni mwa vilabu vya England.

Manchester City, Chelsea and Arsenal wanaonekana ndio watakaokuwa wa kwanza kuanza mbio za kumuwania mcameroon huyo.
Hata hivyo Eto'o aliwahoi kukaririwa akisema angependa kufanya kazi na Gunner's coach Asenal Wenger.

1 comment:

  1. Karibu sana Etoo Emiratee huenda ukatufuta machozi wadau.

    ReplyDelete