Search This Blog

Tuesday, June 7, 2011

JACK RODWEL JINSI YA KUCHEZA 'BOX TO BOX'


Jack Rodwel ni vipaji vipya katika ligi kuu ya Uingereza, anacheza katika timu ya taifa ya England under 21 na anaichezea klabu ya Everton katika nafasi ya kiungo.Katika siku za hivi karibuni Sir Alex Ferguson kwa pamoja na Arsenal Wenger wamekuwa wakipigana vikumbo kutaka saini ya mchezaji huyu. Everton's midfielder amekuwa kwenye kiwango bora msimu huu na hapa anaelezea hatua sita za namna ya kucheza na kutawala uwanja mzima (Box to Box midfielder - Kiungo anayecheza mchezo wa kushambulia na kukaba). 1:HIFADHI NGUVU "Kama unataka kucheza kwa kutawala kwa kucheza box to box inabidi uifadhi nguvu zako wakati wa kukimbia, ili kufanya hivyo unatakiwa kuji-position vizuri mapema ili uweze kuepuka kupoteza nguvu kwa kuahangaika uwanja mzima haswa haswa katika mechi kubwa, hivyo ni vizuri kukaa kwaenye nafasi nzuri ili uweze kuifadhi nguvu."

2:USITABIRIKE

“Kama unacheza dhidi ya kiungo/viungo wanaocheza kwa mtindo wa Box to box, jaribu kuwazuia wao wasicheze kwanza halafu usitabirike.Kipindi cha kwanza zuia kwenda sana mbele ili adui wako afikiri kuwa upo pale kumkaba yeye na kucheza mchezo wa kuzuia zaidi, halafu kipindi cha pili, ukizingatia na mchezo unavyokwenda, anza kufanya mashambulizi na kumfanya adui yako achanganyikiwe asijue nini utafanya baadae."

3:CHUKUA TAHADHARI

“Kama unakuwa ndio unaongoza ukabaji inabidi udhibiti mbio zako za kushambulia, lakini kuna muda muda inabidi ucheze kamari.Msimu uliopita dhidi ya Manchester United tukiwa nyuma kwa 2-1 niliingia na jukumu langu lilikuwa ni kusaidia kupata goli ndani ya dakika 5 zilizokuwa zimebaki, lakini nilipopata mpira nikiwa katikati nilitafuta nafasi na nikafunga goli lililomaliza mchezo."

4:LINDA UKUTA WAKO

“Zingatia katika kuvunja mashambulizi na kuwazuia washambuliaji kupata mipira kwenye miguu yao.Kiungo mpinzani atataka kumpa mshambuliaji wake mpira hivyo unachotakiwa kufanya ni kugeuka kwa haraka kuipata pasi yake ya pili.Ikiwa mtu Wayne Rooney akiingia ndani , tulia, kaa kwenye nafasi yako na jua kwamba hauwezi kupata kupata mpira.Unachotakiwa kufanya ni kulinda mabeki wako wa nne kwa nyuma kwahiyo kama Rooney atataka kurudi nyuma acha mabeki wako wacheze nae, akiingia ndani inakuwa kazi yako."

5:CHELEWA KUINGIA NDANI YA BOKSI

“Kama unajua wapi mawinga wako watapeleka mpira, mara 9 kati ya 10 utaipata krosi.Ikiwa mabeki wanakuangalia unatakiwa kuwahi kupiga kichwa mpira hivyo atakuwa anarudi kinyumenyume kuelekea kwenye penalty box hivyo nawe ingia kwa nguvu, shusha bega lako halafu kaa kwenye nafasi yako kabla ya adui wako hajafika pale halafu unaweza ukafunga."

6:UNDA USHIRIKIANO

“Jenga uelewano wa na kiungo mwenzio, chezeni kwa kwa nguvu.Nikiwa nacheza na Tim Cahil mpira ukiwa unaenda pembeni najua natakiwa kurudi nyuma na kulinda nafasi yangu katika kiungo cha chini ili ku-balance team.Nikiwa nacheza na Marouane Fellaini yeye huwa analinda mimi nakwenda kushambulia halafu nakuwa namwachia mipira ya mwisho Mikel Arteta na mimi nabaki kuwalinda washambuliaji."

No comments:

Post a Comment