Search This Blog

Thursday, June 16, 2011

HATUMUUZI NEYMAR - SANTOS WAIAMBIA CHELSEA


CHELSEA wameambiwa kuwa wanapoteza muda wao kwa kujaribu kumsajili Brazilian wonder kid Neymar.
Onyo hilo limetolewa na na raisi ywa klabu ya Santos Luis Avaro de Oliveira.
The Blues walimtuma na kumpa madaraka wakala maarufu wa wachezaji Pini Zahavi kwenda Brazil kufungua majadiliano ya kumsaini Neymar Chelsea, lakini Santos kupitia raisi wake wameweka wazi kuwa kinda wa hauzwi ingawa Chelsea wanaamini hiyo janja tu Santos kutaka kupandisha bei ya Neymar.
De Oliveira amesisitiza kuwa,:
" Kwa sasa tupo katika maongezi na wadhamini wetu wakubwa waweze kutufanikishia mpango wa kuhakikisha Neymay anaendelea kuwa mchezaji wetu kwa kumpa dili nzuri ya kueleweka.Kumekuwa hakuna ofa mpya iliyokuja ndani ya siku kadhaa zilizopita lakini zikija bado tutazikataa."
Neymar mwenyewe amezungumza na kusema kuwa "Ndoto ya wabrazili wengi ni kucheza ulaya na kwangu haipo tofauti."

No comments:

Post a Comment