Search This Blog

Wednesday, June 15, 2011

EDMUNDO KWENDA JELA KWA KESI YA MAUAJI



Jaji wa mahakama ya jiji ya Rio De Jeneiro Eduardo Carvalho de Figueirdo ametoa amri ya kukamatwa kwa straiker wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Edmundo kwa kusababisha ajali ya gari ambayo ilichukua maisha ya watu 3 mwaka 1995.
Edmundo ambaye aliwakutwa na hatia ya kufanya mauji bila kukusudia mwaka 1999., lakini akakata rufaa na akashindwa lakini hatua za kisheria dhidi yake hazikuchuliwa mpaka jana Jumanne Jaji Eduardo alipotoa amri ya kukamatwa kwake.
Mawakili wa Edmundo wamesema watakata rufaa tena.Kwa sasa bado Edmundo hajakamatwa.
Edmundo kwa sasa ana umri wa miaka 40 aliwahi kuzichezea klabu 13 tofauti akianzia Vasco Da Gama, Flamengo, Palmeiras, Corinthians, Napoli, Cruzeiro, Fluminense, Fiorentina, Santos, Tokyo Verdy, Urawa Red Diamonds, Nova IguaƧu, na Figueirense.
Katika kipindi cha hivi karibuni Edmundo amekuwa ni commentator wa television nchini Brazil.


JIKUMBUSHE KIDOGO UWEZO WA EDMUNDO THE ANIMAL

No comments:

Post a Comment