Search This Blog

Monday, June 6, 2011

Hassan Shehata aachia ngazi

Hassan Shehata aachia ngazi



Chama cha soka cha Misri Kimekubali barua ya kocha Hassan Shehata kujihuzulu wadhifa wa kocha wa timu ya taifa baada ya kulazimishwa sare na bafana bafana mwishoni mwa juma.


Mafanikio ya HASSAN SHEHATA
2001-2003: alikiongoza kikosi cha umri chini ya miaka 20 kufuzu kombe la dunia mnamo mwaka 2003
• 2004: Alichaguliwa kuwa kocha wa timu ya wakubwa ya taifa
• 2006: alikiongoza kikosi cha misri kutwaa ubingwa wa Africa kwenye ardhi ya nyumbani kwa kuifunga ivory Coast kwa mikwaju ya penalti
• 2008: aliiongoza timu kuchukua ndoo ya pili mfululizo ya kombe la mataifa ya bara la afrika
• 2009: alipoteza nafasi ya kufuzu fainali za fifa za kombe la dunia mbele ya mahasimu Algeria
• 2010: aliiongoza Misri kuweka rekodi ya kuchukua mara tatu mfululizo kombe la mataifa ya Afrika kwa kuifunga Ghana kwenye fainali.
• 2011: anajihuzulu wadhifa wa kuifundisha timu ya Taifa baada ya kuanza vibaya kufuzu fainali za kombe la afrika mwaka wa 2012.

No comments:

Post a Comment