KAMPUNI YA SIMU YA AIRTEL TANZANIA KWA KUSHIRIKIANA NA KLABU YA MANCHESTER UNITED LEO IMEZINDUA PROGRAM YA KUIBUA VIPAJI VYA SOKA NCHINI TANZANIA KUANZIA NGAZI YA CHINI HADI TAIFA.
PROGRAM HIYO INAFAHAMIKA KAMA AIRTEL RISING STARS INAJUMUISHA BARA ZIMA LA AFRICA ILI KUWEZA KUTOA NAFASI KWA WANASOKA CHIPUKIZI CHINI YA UMRI WA MIAKA 17 KUONYESHA UWEZO WAO MBELE YA MAWAKALA WA SOKA NA MAKOCHA ILI KUWEZA KUPATA FURSA YA KUJIENDELEZA ZAIDI.MPANGO UNAWAHUSISHA WASICHANA NA WAVULANA.
PROGRAM HII HAPA TANZANIA ITAFANYIKA KATIKA MIKOA YA DAR, MOROGORO, MWANZA NA ARUSHA IKISHIRIKISHA VIJANA ZAIDI YA 500 AMBAPO WAWILI KATI YA HAO WATACHAGULIWA KUJIUNGA NA KLINIKI YA SOKA ITAKAYOFANYIKA NCHINI GABON NA TANZANIA CHINI YA USIMAMIZI WA JOPO LA MAKOCHA KUTOKA MANCHESTER UNITED.
PIA KAMPUNI YA AIRTEL AMBAYO INA MKATABA WA KUIDHAMINI MANCHESTER UNITED KWA MIAKA 4 IMESEMA ITAFANYA KAZI NA WIZARA YA HABARI,VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO PAMOJA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA(TFF) KATIKA KUTEKELEZA PROGRAM HII YA AIRTEL RISING STARS.
No comments:
Post a Comment