Search This Blog

Friday, June 10, 2011

DONE DEAL - FERGIE AMNYAKUA ASHLEY YOUNG KWA £20 MILLION


ALEX FERGUSON amemalizana na Aston Villa baada ya kumnyakua Ashley Young kwa ada ya £20 mIL. jana usiku.

Baada ya usajili huuMan United sasa watakuwa wametumia kiasi cha £55m wakiacha mbali wapinzani kwenye kivuli chao.

Kuwasili kwa Young kumekamilisha usajili wa Fergie kufikia £55m akiwa bado anaendelea kukiimarisha kikosi chake.

Ashley Young alifaulu vipimo vya afya katika kliniki iliyopo katika uwanja wa mazoezi wa United Carrington halafu akatia saini mkataba wa kuichezea Man U kwa miaka minne, na sasa anaungana na Phil Jones ambaye alijiunga na United kwa £16m jumatano, na pia dili lingine la kumsaini David de Gea lenye thamani ya £18M linasubiri saini tu.

Ujio wa Ashley mwenye uwezo wa kucheza kama winga au mshambuliaji wa pili atakuwa nyongeza tosha katika kuifanya United kuwa na safu kali ya ushambuliaji, ingawa pia uwepo wake Old Trafford unaweka shakani nafasi ya Luis Nani .



1 comment:

  1. daah man united wanazi kuwa imalaa cjui cc arsenil vivi

    ReplyDelete