Search This Blog

Wednesday, June 8, 2011

BREAKING NEWS - PHIL JONES KUFANYIWA VIPIMO LEO NA KUJIUNGA NA MAN UTD


Blackburn Rovers defender Phil Jones ameonekana jijini Manchester na kwa mujibu wa Skysports leo baadae atafanyiwa vipimo vya afya na Manchester United.

Inaaminika Man United wamemchukua Jones kwa paundi millioni 16 na wameshakubaliana na Rovers.

Jones ambaye amepewa na United mkataba wa miaka 5 alitakiwa kuondoka na timu ya vijana ya England U21 kuelekea Denmark jana lakini aliharisha ili aweze kukamilisha uhamisho na United na anategemewa kuondoka leo usiku kuelekea Denmark kujiunga na wanzake.

Kwa usajili huu United wamewapiga bao mahasimu wao wakubwa Liverpool ambao nao walikuwa karibu mno kufanikisha kumsajili Jones.

No comments:

Post a Comment