Search This Blog

Saturday, May 14, 2011

YANGA YAKATAA UJIO WA BIRMINGHAM.



Klabu ya yanga ya Dar es salaam imesema haitaki kuhusishwa katika maandalizi ya kuileta timu ya BIRMINGHAM CITY ya uingereza lakinai itakua tayari kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu hiyo endapo itafanikiwa kufanya ziara yake yakuja nchini mapema mwezi ujao.

Mwenyekiti wa yanga Lloyd Nchunga alisema jana kwamba klabu yake imefikia maamuzi hayo baada ya kuona kwamba ni kiasi kikubwa mno cha fedha (sh.bilioni 2.7)kinahitajika ilikuileta timu hiyo,jambo ambalo ni ndoto kwa yanga na simba kumudu gharama hizo zilizoelezwa.

No comments:

Post a Comment