Search This Blog

Wednesday, May 25, 2011

TFF KUKUTANA NA MAKOCHA NA WAAMUZI.



Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF kupitia kurugenzi yake ya ufundi inatarajiwa kukutana na makocha pamoja na waamuzi wote wa soka wanaoishi jijini Dar es salaam mwishoni mwa juma hili.

Boniface Wambura Afisa Habari wa TFF amesema kwamba mkutano huo ni muhimu ambao utasimamiwa na Mkurugenzi wa ufundi wa TFF Sunday Kayuni ukiwa na lengo la kusaidia maendeleo ya soka la hapa nyumbani.

No comments:

Post a Comment