Search This Blog

Wednesday, May 25, 2011

SIMBA SPORTS CLUB KUONDOKA LEO USIKU.



Wawakilishi wa Tanzania Bara katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika wekundu wa Msimbazi Simba Sports Club wanatarajiwa kuondoka nchini leo usiku kuelekea Misri kwa ajili ya pambano lao dhidi ya Wydad Casablanca.

Simba wanatarajiwa kuondoka na msafara wa kikosi cha watu 27 kitakachoongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF Muhsin Balabuu.

Wachezaji watakaokwea pipa usiku huu ni Juma Kaseja Juma, Ally Mustapha, Salum Kanoni , Ramadhani Haruna Shamte, Juma Jabu, Juma Nyosso, Amir Maftah, Kelvin Yondani, Hillarry Echesa, Mohamed Banka, Jerry Santo, Nicholas Nyagawa, Salim Aziz Gilla, Shija Mkina, Ally Ahmed Shiboli, Mussa Hassan Mgosi, Amri Kiemba pamoja na Emmanuel Okwi


Viongozi watakaoambana na timu hiyo ni mwenyekiti Ismail Aden Rage, Makamu mwenyekiti Geofrey Nyange Kaburu, katibu wa timu Evodius Mtawala, Joseph Matore, Cosmas Kapinga, Mosses Basena, Amatre Richard, Abdallah Kibaden Mputa na Iddi Pazi,



Ama kwa upande mwingine Shirikisho la mpira wa Miguu Tanzania TFF kupitia kwa Rais wake Leodgar Tenga limeitakia kila la Kheri Simba ili iweze kufanya vizuri katika mchezo huo.

Tenga ameeleza kwamba ushindi wa Simba katika mchezo huo ni muhimu kwa soka la Tanzania kwa kuwa wataitangaza zaidi nchi endapo watafuzu katika hatua ya makundi ya michuano hiyo.




No comments:

Post a Comment