Search This Blog

Saturday, May 14, 2011

SIKUMTUKANA MARCELO-BUSQUETS.


Kiungo wa mabingwa wa La Liga, Sergio Busquets amejitokeza hadharani na kupinga madai ya kwamba alimtukana beki wa Real Madrid Marcelo kwa kumuita nyani katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya kwanza ya Champions League iliyozikutanisha Barcelona na Real Madrid kwenye uwanja wa Santiago Bernabeu.
Spanish Midfielder amepinga madai baada ya kutangaza kwamba wamefungua kesi ya nidhamu dhidi yake.
Real Madrid walalamika kwa UEFA kwamba Busquets alimwita Marcelo “MONO” (nyani), na kutoa video ambayo inamuonyesha Barcelona midfielder akiongea huku akiwa ame-cover mdomo wake na kiganja cha mkono.
Msemaji wa Barcelona pia amepinga madai hayo ya Real Madrid akisema ni madai hayo ni ya uongo na Madrid wana nia mbaya dhidi ya timu na mchezaji wao.
Barcelona wanatarajiwa kuwasilisha utetezi wao Leo (Ijumaa) na kama Busquets atapatikana na hatia aanaweza kusimamishwa hivyo kukosa fainali ya Champions League dhidi ya Manchester United tarehe 28 mwezi huu katika uwanja wa Wembley-Uingereza.

No comments:

Post a Comment