Search This Blog

Thursday, May 26, 2011

KLABU YA YANGA IPO KATIKA MCHAKATO WA KUTAFUTA SULUHU.



Klabu bingwa ya kandanda ya Tanzania bara Dar es salaam Young Africans, ambayo ilifungiwa na baraza la vyama vya kandanda vya ukanda wa Afrika ya mashariki na kati kushiriki katika michuano yake ya ukanda huu, sambamba na kupigwa faini, ipo kwenye mchakato wa kutafuta suluhu.

Miamba hao wa Tanzania bara, walifungiwa miaka miwili iliyopita na Cecafa, na kupigwa faini ya dola za kimarekani elfu thelathini na tano, kwa kitendo chao cha kugomea mechi ya kusaka mshindi wa tatu wa michuano hiyo ilipofanyika jijini Dar es salaam dhidi ya mahasimu wao Simba.



Kwa mujibu wa afisa wa habari wa klabu hiyo Louis Sendeu anasema kwamba, walikuwa kwenye mazungumzo na katibu mkuu wa Cecafa Nicholaus Musonye, juu ya kupunguziwa adhabu hiyo, hasa baada ya kuona kwamba sasa muda umefika kwa wao kuwa na umuhimu wa kushiriki katika michuano hiyo, na zaidi wanashindwa kuulaumu uongozi uliopita.

Kwa upande wa pili, suala la usajili ndani ya klabu hiyo bingwa ya Tanzania bara, Sendeu anasema kwamba wanakwenda vizuri, na wamehakikisha wanafuata yale yaliyoachwa na kocha mkuu wa klabu hiyo, Sam Timbe aliyeko nyumbani kwao nchini Uganda.

Pia amezungumzia juu ya suala la kiungo wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima, na mnamo mwezi ujao wanandinga wa klabu hiyo wanatarajiwa kuanza kuwasili kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu ya kandanda ya Tanzania bara kwam msimu wa 2011/12 na michuano ya kimataifa baadae.


Upande mwingine, shirikisho la soka la Tanzania TFF limesema kwamba, kamati yake ya utendaji haiwezi kuiombea msamaha Young Africans, kutokana na makosa waliyofanya, ya kugomea mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Raisi wa shirikisho la soka la Tanzania TFF, Leodgar Chilla Tenga anasema kwamba, Young Africans wanatakiwa kuomba msamaha wenyewe, kwani ukivunja kanuni utaadhibiwa, lakini kama watakuwa wameomba msamaha basi watakuwa wamefanya jambo la busara sana, na moja kati ya mambo mabaya yaliyokuwa yamefanyika nchini katika soka, ni kitendo kile, lakini kama Cecafa watakaa.



No comments:

Post a Comment