Search This Blog

Wednesday, May 25, 2011

ABROMOVICH MKOSEFU WA FADHILA NA ANAHARIBU SOKA-CHAMA CHA MAKOCHA ENGLAND


Roman Abramovich na Chelsea jana usiku walitupiwa na madongo ya kukosa fadhila na kuwa ni waaribifu wa mchezo wa soka baada ya kumfukuza Carlo Ancelotti.
Chelsea walimtimua Anceloti saa moja baada ya mechi ya mwisho ya EPL miezi 12 baada kukiongoza kikosi cha The blues kuchukua makombe mawili, na sasa chama cha makocha wa England kupitia CEO wao wamesema Chelsea wamekosa heshima na wanaharibu hadhi ya mchezo wa soka.
"Jinsi walivyomfuta kazi Carlo ilikuwa ni ukosefu mkubwa wa adabu, mwakilishi wa Chelsea alimfuata Ancelotti katika korido za kuingilia uwanja wa Everton na kumpa ujumbe wakufukuzwa kutoka kwa Boss, kiukweli haikuwa sawa na inaharibu hadhi ya mchezo na nafikiri Mr.Abromovich inabidi awe muangalifu na watu wanaomshauri kwasababu wanatumia njia mbaya sana kuendesha klabu, anahitaji kuwa na heshima kwa historia na utamaduni wa mchezo."
"Nafikiri mpaka sasa wameshafukuza makocha saba ndani ya miaka nane, ni dhahiri mmiliki analitaka kombe UCL.Carlo ni mtu mwenye heshima na hadhi yake, na anaweza kuwa moja watu wazuri tuliowahi kuwa hapa hakupaswa kutendewa vile"- alisema Richard Bavan.

No comments:

Post a Comment