Search This Blog

Monday, July 11, 2011

GARY NEVILLE: NATUMAINI SNEIJDER ATATUA OT



Mchezaji wa zamani wa Manchester United Gary Neville anaamini Wesley Sneijder atatua Old Trafford this summer.

United wamekuwa wakihusishwa sana na usajili wa Sneijder ambaye aliisaidia Inter Milan kushinda treble mwaka 2010, pamoja na kuisadia Uholanzi kufika fainali ya WOZA 2010.

Kauli ya Gary Neville inafuatiwa baada ya last week kocha msaidizi no.2 wa United Rene Meulensteen kusema haoni mchezaji mwingine sahihi wa kujiunga na Red Devils kwa wakati huu kama sio Wesley Sneijder.

Alisema: “Sneijder ni mchezaji mzuri ambaye amewahi kucheza katika timu kubwa kama Real Madrid na sasa Inter haitonishangaza akijiunga nasi hapa.

Ana uwezo wa kucheza mahali ambapo ni vigumu kucheza, anaweza kufunga mabao na kutoa assist kwenye mechi muhimu.

Utakuwa ni usajiri muhimu akijiunga na United, lakini na hakika zipo timu nyingine zinamfuatilia.

Natumai Manchester watampata japo sina uhakika na suala hilo.” –alimaliza Gary Neville

Wakati huo huo Wesley Sneijder amezungumzia usajili wake kwenda United huku akisema atahuzunika kama Inter wataamua kumuuza.

“Ningependa kuendelea kubaki hapa, nina team-mates wazuri sana.Mke wangu Yolanthe na mimi tunaipenda Inter, mashabiki na nchi ya Italia.

Ikiwa klabu itaamua kuniuza, nitaenda popote watakaponipeleka lakini itaniuma sana.

Mimi na familia yangu tumekuwa tukijisikia vizuri tukiwa hapa, na nitaumisi sana mji wa Milan pamoja na Inter.Lakini soka ndio lipo hivyo, kipindi ambacho nilipouzwa na Real Madrid kuja Inter, nilitamani kuendelea kubakia nchini Hispania.

Chochote kitakachotokea, kitatokea.” – alimaliza Sneijder.

TANZANIA YAZICHAPA KENYA MABAO 7 - 1 NA CAMEROON 13 - 3.

Kikosi cha watanzania waishio nchini Sweden kimeanza kwa kishindo kuutetea ubingwa wa Africa Challenge Cup,mashindano yanayoandaliwa na chama cha 'the Sports Association of Afro-Scandinavians ' (SAAS).Tanzania ni mabingwa watetezi na jumapili ijayo inacheza na burundi. kikosi cha Tanzania kinaongozwa na Nyota kama Shekhan Rashid, Aboubakary Mkangwa ,Joseph Kaniki 'Golota' ,kijana Richard Messi na William John (captain) Chini ya Kocha wao NYUPI Phillip.


KIKOSI CHA KENYA

NAHODHA WA TANZANIA KIUNGO WA ZAMANI WA SIMBA WILLIAM JOHN



KIKOSI CHA WATANZANIA WAISHIO NCHINI SWEDEN
HUYU ANAITWA RICHARD MAARUFU KWA JINA LA MESSI.
HUYU NI JOSEPH KANIKI ' GOLOTA' MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA SIMBA.

UNITED WAKIWA SAFARINI KWENDA KUPAMBANA NA NGASSA





VINCENT KOMPANY KUMVUA KITAMBAA TEVEZ


Vincent Kompany anatarajiwa kutangazwa kuwa nahodha mpya wa Manchester City hata kama Carlos Tevez atabaki in Eastlands club.

Kompany ambaye alikuwa akishika nafasi ya unahodha kipindi Tevez alipokuwa amekosekana katika baadhi ya mechi msimu uliopita ndani kikosi cha Man City, na sasa ikiwa ni baada ya wiki moja kupita tangu Tevez awasilishe ombi la kutaka kuondoka vyanzo vya habari kutoka ndani ya klabu hiyo zinasema Vincent Kompany anapewa nafasi kubwa ya kupewa kitambaa cha unahodha.

Tevez alipewa uongozi baada ya Kolo Toure, mwanzoni mwa msimu uliopita katika hali ya kuhakikisha mchezaji wa raia wa Argentina anabaki ndani ya City of Manchester.

Lakini, kipindi Tevez akiwa kiongozi mzuri uwanjani, kugombana kwake na kocha Roberto Mancini, kuomba kuondoka mara mbili kumemfanya asiaminike mbele ya mashabiki wa timu hiyo.

DE JONG: MAN CITY TUMEWAZIDI CHELSEA KWA KUCHUKIWA


Nigel de Jong amesema anafahamu kuwa Manchester City ndio inayochukiwa zaidi duniani.

The Dutchman anahisi City imewabadili Chelsea kama timu inayochukiwa zaidi kama ambavyo mashabiki wanavyoonyeshaa kupenda timu yao ifungwe.
Akiongea na gazeti la Manchester Evening News alisema."Naamini tumekuwa tukichukiwa sana, kitu ambacho Chelsea wameshakutana nacho.Kipindi tukiwa uwanjani kwenye mechi huwa naona kabisa chuki ya mashabiki wa uwanjani dhidi yetu, hakuna anayependa sisi tufanikiwe.
Chuki ya watu dhidi ya Chelsea zilipungua waliposhinda ubingwa na naamini kwetu itakuwa hivyo.
Baada ya kushinda kombe la FA niliona mabadiliko kidogo."

NASRI NA FABREGAS HAWAENDI KOKOTE


Manager wa klabu ya Arsenal ameendelea kujigamba kuwa ameshinda vita ya kuwabakiza majembe yake mawili viungo Cesc Fabregas na Samir Nasri.

Akiongea na press mara baada ya kikosi chake kutua in Kuala Lumpur kwenye ziara ya mashariki ya mbali, Wenger alisema :

"Samir Nasri ataendelea kuwa hapa msimu ujao, lakini kuhusu kuongeza mkataba mpya hilo siwezi kulitolea uamuzi peke yangu."

Akiongelea kuhusu sakata la mchezaji na naohodha wa timu hiyo Gunner's boss alisema:

*Naamini Cesc atabaki hapa, Fabregas anaipenda klabu hii na matumaini yangu tutafanikiwa kumbakisha hapa.

Tunafahamu kuhusu story ya Barcelona imekuwa ikiendelea kwa miaka sasa na inabidi tuachane hili suala ili tujipange na msimu ujao tukiwa na imani tutafanya hivyo tukiwa na CESC.


Huku Fulham, Borussia Dortmund and Sporting Lisbon wakivutiwa na Bendtner, na Atletico Madrid na Malaga wakiongoza mbio za kumnyakua Almunia, Wenger alikiri uwezekano wa kuondoka kwa wachezaji hao unabaki kwenye suala la muda tu.

"Wachezaji wote hawa wataondoka, kwa sasa wanaongea na klabu zinazowahitaji."

Pia akiongelea kuhusu uhamisho wa mchezaji kutoka Ivory Coast Gervinho, Wenger alisema: "Ni kweli Gervinho amejiunga nasi, na sasa yupo London akifanya mazoezi.Alirudi kutoka kwenye mapumziko na amesaini.Alifanya vipimo Alhamisi lakini tulimpa ruhusa kwenda kwa familia yake ili kuweka mambo sawa kwa siku mbili.

Alirudi London jana na ameanza mazoezi ya kujiweka sawa in London Colney.Ni mchezaji rasmi wa Arsenal sasa, lakini niliamua kumuacha kwenye ziara hii kwa sababu hakuwa amefanya mazoezi kabisa."



JINSI WACHEZAJI WA YANGA NA SIMBA WALIVYOCHEZA KWENYE FAINALI YA KAGAME CASTLE CUP.

Yanga.
1. Yaw Berko
Hakusumbuliwa sana kwa sababu washambuliaji wa Simba mara nyingi hawakupeleka mipira ambayo ingembugudhi na kumpa wasiwasi kama ile ambayo yanga walipeleka kwenye lango la Simba.( 7/10 )


2.Shadrack Nsajigwa .
Kama ilivyo kawaida yake , alikuwa akiongoza kwa mfano , “work ethic” yake ilikuwa juu, na hakupata tabu kuwamudu viungo wa Simba na alipata wakati mwepesi kumkaba Salum Machaku ambaye hakuwa na ujanja wa kumpita . ( 7/10 )

3.Oscar Joshua .
Kwa nguvu nyingi alizokuwa anatumia ungeweza kudhani kuwa angeigharimu timu yake lakini haikuwa hivyo kwani ali-win “Battles” nyingi sana na viungo wa Simba na haishangazi kuona kuwa upande wake ulikuwa salama kwa muda mrefu wa mchezo.( 7/10 )

4.Nadir Haroub Cannavaro.
Alikuwa kwenye kiwango chake cha siku zote ambapo alikuwa anatumia nguvu na akili pale inapohitajika, na jinsi mchezo ulivyokuwa kwa ujumla ulikuwa unampa wakati mwepesi kazini japo alionyesha “lack of professionalism” kwa kumchokoza Haruna Moshi ili kumtafutia kadi , pia alikuwa na wakati ambao tatizo lake kubwa ambalo ni kukosa mawasiliano na mabeki wenzie lilionekana na lingeweza kuidhuru timu yake . ( 8/10 )


5.Chacha Marwa.
Alicheza kwa ujasiri mkubwa kama ambavyo ametokea kuwa mtu wa kutegemewa kwenye “kumi na nane” ya Yanga . Hakuwa na papara sana na wala tatizo la kukosa mawasiliano baina yake na beki mwenzie wa kati Cannavaro halikuonekana sana na halikuonekana kwa sababu yake. ( 7/10 )

6.Nurdin Bakari.
Kama kuna mtu ambaye alikuwa nyota wa mchezo tena kwa alama zote basi Nurdin anaqualify kuwa mtu huyo , alikuwa ana-enjoy kucheza soka na alikuwa akifanya mambo bila papara ambazo wachezaji wanakuwa nazo wakati wa mechi kubwa kama hii , alikuwa na uhuru mwingi sana eneo la kati kati ya uwanja . Kuna mambo makuu matatu ambayo yalimsaidia Nurdin , kukosekana kwa Jerry Santo, kutoka mapema kwa Mwinyi Kazimoto na pia kuwa nje ya mchezo kwa aliyeingia kuchukua nafasi ya Mwinyi, Mohamed Banka ambaye mchezo wake uliokosa mwelekeo na malengo ulimpa faida kubwa Nurdin bakari.( 9/10 )


7.Godfrey Taita.
Kwa upande wake kidogo alikuwa anakosa maarifa ya kumkabili Amir Maftah ambaye mara nyingi huwa ana tatizo la kukosa umakini kwenye kukaba , hakuwa na madhara mengi kwa beki ya Simba na krosi zake zilikuwa haziongei kwa maana ya kuwa na madhara kwa mpinzani na kuwa na faida kwa washambuliaji wake aliokuwa anawalisha. Kama walinzi wengi tulio nao kweye nafasi yake alikuwa anatumia nguvu nyingi kuliko maarifa labda ni kutokana na kuzoea kucheza kwenye defence mara kwa mara na pia yawezekana alikua na fatigue baada yak kucheza dakika 120 za nguvu kwenye mchezo wa nusu fainali. ( 6/10 )

8.Juma Seif Kijiko .
Hakuna aliyekuwa anajua mengi kuhusu mchezaji huyu kabla ya michuano hii japo alikuwepo Yanga na alicheza baadhi ya mechi za ligi kuu msimu uliopita na nyingi alikuwa benchi . Ameleta aina tofauti ya mchezo ambao haupo Yanga , ana uwezo mkubwa wa kumiliki mipira kwa kujiamini kwa hali ya juu na ni dhahiri kwamba kama asingeumia basi pengine Rashid Gumbo asingeingia kwa sababu kabla ya hapo hakuna mengi aliyoyafanya ambayo ungeyaita makosa alikuwa akiuficha mpira vizuri na kwa uhakika wa hali ya juu sana na alikuwa akitoa challenge kubwa kwa viungo wa Simba ambao walikuwa wakimiliki sana mipira . ( 7/10 )



9.Davis Mwape .
Mwape ni mshambuliaji asilia , mtu mwenye nguvu nyingi na ni mjasiri asiyekata tamaa, tatizo kubwa ambalo Yanga wameendelea kulifanya juu ya mchezaji huyu ni kutocheza kwa ajili yake . Kwenye mchezo dhidi ya Simba Mwape alicheza nje ya eneo la kumi na nane na hapa huwezi kuona madhara yake kwa mpinzani japo kuna nyakati ambazo alikuwa akiwatisha mabeki wa Simba hasa kwa mipira ya krosi lakini tofauti na hapo ni kama hakuwepo mchezoni na siku ambayo Yanga watagundua njia ya kumchezesha Mwape basi watakuwa wanafunga magoli engi sana na si kumlazimisha acheze nafasi ambayo analazimika kudrible wakati hiyo si kazi yake aliyozaliwa kufanya uwanjani . pia ‘work rate’ yake ilikua juu mno. ( 7/10 )

10.Jerry Tegete .
Kama ilivyo Mwape Tegete alikuwa anachezeshwa “out of position” na alijitahidi kwa kiasi kikubwa sana ku-adopt kwa jukumu alilopewa na alikuwa akiwatoa mabeki wa Simba nje ya eneo na kutengeneza mashimo ambayo kama Yanga wangekuwa makini yangekuwa mashimo ambayo yangewapa magoli mengi . Kimsingi Tegete ni mtu ambaye anapaswa kutumia akili nyingi sana kuwavizia wapinzani na kutafuta njia ya kufunga na si kutafuta njia ya kuwaondoa mabeki nje ya eneo ( withdrawn position ) japo kwa jukumu alilopewa alilifanya kwa ukamilifu .( 8/10 )

11.Kiiza Hamis .
Kiiza ni mchezaji mjanja sana maybe muda wowote anaweza kufanya kitu chenye faida kwa timu yake , ukiacha Nurdin Bakari Kiiza ni mtu ambaye aliwasumbua sana Simba na alikuwa anahaha uwanja mzima kutafuta nafasi na kupenyeza mipira kwa wenzie , pengine mchezo usingekuwa kama ulivyokuwa kama asingekuwepo . alifunga bao ambalo sidhani kama kweli alikua ameotea. ( 7/10 )

Walioingia .
12.Rashid gumbo .
Ni kama alikuwa na deni la kuwalipa Yanga na wakati huo huo alikuwa na kisasi cha kuwalipizia Simba , alimiliki sana mipira eneo lake la katikati ya uwanja na alirejesha “partnership” na Nurdin na kilichomongezea alama kwenye mchezo wa fainali ni krosi yake ambayo ilikutana vyema na kichwa cha Keneth Asamoah ambaye aliukwamisha mpira wavuni na kuipa Yanga ubingwa . ( 7/10 )

13.Keneth Asamoah.
Aliingia kuchukua nafasi ya Jerry Tegete ambaye alitoka wakati wa muda wa nyongeza. Kwa wale waliodhani kuwa Asamoah ni garasa ambalo Yanga imekula hasara kulisajili basi Asamoah amewajibu kwa njia bora ya goli safi ambalo bila shaka limemaliza ubishi wake. ( 7/10 )


Jullius Mrope .
14.Aliingia kuchukua nafasi ya Godfrey Taita na hakuleta “impact” kubwa kwa sababu hakumpa tabu Amir Maftah kwenye upande wake na kilichomuokoa ni ushindi ambao Yanga iliupata. ( 6/10 )

Kocha , Sam Timbe .
Falsafa yake ya kucheza soka la matokeo zaidi imeonekana kuinufaisha Yanga na amefaulu kuandika historia ya kipekee kwa kutwaa ndoo akiwa na timu ya nne , soka lake la moja kwa moja ambalo lina madhara kwa mpinzani limeonekana leo na ndio limeipa Yanga ubingwa na anakuwa kocha gwiji wa michuano na ukanda huu wa Cecafa.

Walivyocheza Wachezaji wa Simba.
1.Juma Kaseja.
Alisimama vizuri langoni japo walinzi wake hasa mlinzi wa kulia Cholo alikuwa anamuweka hatarini kwa kuruhusu hatari nyingi zipite upande wake na hata goli lilipitia huko . Kwa muda mrefu hakuwa mchezoni kwa kuwa mpira ulikuwa ukibutuliwa hovyo na kila timu na pia walinzi wake wa kati walikuwa makini sana kuondoa hatari nyingi langoni mwake . (7/10)

2.Nassoro Cholo.
Kwa mchezo wa jana unaweza kusema kuwa mojawapo ya watu ambao waliigharimu Simba alikuwa cholo , alikuwa akijitahidi kuwakabili viungo wa Simba lakini hakuwa akifanya hivyo kwa kutumia maarifa na mara nyingi alikuwa akisababisha faulo ambazo zilikuwa zilikuwa zinahatarisha lango la Juma Kaseja na pia hakuwa akipandisha mashambulizi kusaidiana na na kiungo aliyekuwa akicheza upande wake . (4/10 )

3.Amir Maftah .
Alicheza katiaka kiwango cha kawaida ambacho huwezi kusema kuwa ni cha juu ama cha chini , kuna wakati alitimiza majukumu ya nafasi yake na kuna wakati alikuwa akipoteza umakini japo alijitahidi vilivyo kuwamudu Godfrey Taita na Jullius Mrope na hawakuleta madhara upande wake labda uchezaji wa Taita ndio ulimfanya awe na wakati mzuri mchezoni . (5/10)



4.Juma Said Nyoso.
Nyoso kama kawaida yake alikuwa moja ya watu ambao walihakikisha lango la kaseja halidhuriki , alikuwa akiwakabili washambuliaji na viungo wa Yanga kwa ujasiri mkubwa na mchezo wake wa kutokuwa na masihara awapo kazini ulimpa alama nyingi mchezoni ,alikuwa aki-link vizuri na mwenzie Yondani . ( 7/10)

5. Kevin Yondani
Kama ilivyokuwa kwa nyoso Yondani hakucheza vibaya , alikuwa makini kwenye eneo lake ambalo mara nyingi halikudhurika na na movement za washambuliaji wa Yanga , dosari pekee kwenye mchezo wake zilikuwa pale ambapo alikuwa anakubali kuvutika kirahisi kwa ujanja aliokuwa anautumia Jerry Tegete wa kumuondoa kwenye eneo lake na kutengeneza mwanya ambao kama washambuliaji wa Yanga wangekuwa makini wangeweza kuwafunga Simba ila alicheza vizuri kwa ujumla japo mchezo wake uliingia dosari pale alipoteleza na kumpa mshambuliaji wa Yanga Keneth Asamoah mwanya muhimu wa kufunga bao lililoipa Yanga ubingwa . ( 6/10)

6.Mwinyi Kazimoto.
Kitu kilichoamua mchezo kwa upande wa Simba ilikuwa ni kuumia kwa Mwinyi Kazimoto ambaye aliipa uhai miubwa sana safu ya kiungo ya Simba , alikuwa na hamu na mpira na alikuwa akiufanya kama anavyotaka , alikuwa aki-penetrate kwenye ngome ya Yanga kwa kujiamini kwa hali ya juu na kutoka kwake kulirejesha pumzi kwenye safu ya kiungo ya Yanga , kwa dakika chache alizocheza hakika alikuwa nyota kwa upande wa Simba .( 8/10 )

7.Shija Mkina .
Kwa dakika alizocheza alikuwa moja ya watu waliokuwa na uhai kwa Simba , kwenye kipindi cha kwanza alitengeneza nafasi mbili za uhakika ambazo kama zingefanyiwa kazi kwa umakini basi matokeo yasingekuwa yale yalioamua mchezo , alikuwa akipanda na kushuka kwa nidhamu ya hali ya juu ambayo itamshawishi kocha yoyote kumpa nafasi kwenye kikosi chake japo kuna wakati ukosefu wa uzoefu wa mechi kubwa ulionekana kumuathiri kwa jinsi alivyokuwa akifanya maamuzi yake akiwa na mpira mguuni, kwa bahati mbaya mechi ilimzidi nyakati za mwisho za mchezo na alitolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Salum Machaku. (7/10 )


8.Patrick Mutesa Mafisango.
Ukimuacha Mwinyi , Shija na Ulimboka mchezaji mwingine aliyeipa Simba uhai ni huyu jamaa toka Rwanda , Mafisango ana akili nyingi sana ambazo hatuzioni kwa wachezaji wetu , anapopata mpira haupotei na pasi zake ni za umeme na si za mkaa , ni mfano halisi wa kiungo anavyotakiwa kucheza , kilichofanya mchezo wake usiwe na madhara kwa Simba ni wenzie kushindwa kuelewa aina ya Soka ambalo Mafisango analicheza kwani kama ingekuwepo “chemistry” kati yake na wenzie basi Simba ingefaidika sana na uwepo wa Mafisango. ( 7/10 )

9.Musa Hassan Mgosi .
Kwa nafasi aliyocheza Mgosi hakuwa na la kufanya zaidi ya yale aliyoyafanya kwa sababu hakulishwa ipasavyo japo kuna nyakati ambazo angeweza kufanya juhudi zaidi na kuipa msaada timu yake na hakufanya hivyo , kinachomgharimu Mgosi ni ukweli kwamba si mshambuliaji wa kuzaliwa , huyu ni kiungo-winga anayelazimika kucheza nafasi ya ushambuliaji na ndio maana huwa anakumbana na lawama za kupoteza nafsi nyingi sana . ( 6/10 )

10.Haruna Moshi Boban .
Haruna ni moja kati ya wachezaji wachache wa ukweli ambao Tanzania inaweza kujivunia kuwa nao , ana vitu vingi vya ziada ambavyo wenzie wengi wanavikosa , alikuwa akitengeneza nafasi nyingi sana kwa Simba lakini shida kubwa waliyo nayo Simba ni kumkosa mtu ambaye anaweza kuzifanyia kazi pasi za kina Haruna na kina Mafisango. Tatizo kubwa la Haruna ambalo litaendelea kumhukumu kwenye soka la miaka ya sasa ni kutokuwa na ujasiri , Haruna ni mchezaji wa kwanza kukubali matokeo na kuweka silaha chini , hili lilionekana kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Al Mareikh na hata kwenye fainali dhidi ya Yanga ambapo alionekana kuchoka mno na sura yake ilikuwa inaonyesha kuwa alikuwa anaomba mchezo uishe haraka ili ajiondolee balaa .( 6/10)

11.Ulimboka Mwakingwe.
Ulimboka alicheza vizuri sana kiujumla, hakuna makosa mengi ambayo aliyafanya ana alidhihirisha ukongwe wake ambapo uzoefu alio nao wa mechi kubwa kama hii ulimsaidia, alikuwa mtulivu na hakuwa na papara nyingi , alijitolea mno kwa timu yake akipanda na kushuka na wakati mwingine “ku-switch flanks” na Shija Mkina jambo ambalo liliwachanganya walinzi wa Yanga , kwa upande wa Simba Uli ni moja ya watu waliocheza vizuri ingawa alikosa bao la wazi kipindi cha kwanza. Lakini pia mpira alioupoteza ndiyo uliozaa bao la Yanga (6/10)


Walioingia.
Mohamed Banka .
Hakika kama ambavyo Nurdin Bakari alichukua sifa ya “man-of-the –match” basi Banka anastahili ile ya “flop-of-the-match”, Banka aliigharimu Simba sana kwa aina yake ya uchezaji ambapo alikuwa mzito sana wa kufanya maamuzi ,alipenda kufanya “dribbling” ambazo hazina maana yoyote , hakuna pasi yoyote inayoongea ambayo aliipiga na mchezo wa Simba uliamuliwa na kuingia kwake ambapo mchezaji aliyekuja kuchukua nafasi ambaye alitoka baada ya kuumia alifanya mengi mno ambayo Banka alikuja kuyaua kabisa . (4/10 )

Salum Machaku.
Salum nbi cmhezaji ambaye bado hajakomaa kuichezea klabu kama Simba , bado jezi nyekundu na nyeupe ni nzito sana mwilini mwake na hatambui majukumu anayokuwa nayo mchezaji wa Simba awapo uwanjani hasa anapokuwa uwanjani kwenye mchezo dhidi ya Yanga , ana mchezo wa kitotona wa kizamani ambao hakika si Tanzania tu hata ulaya hauna tena nafasi , anakaa na mpira bila kuwa na malengo nao, na zaidi ya yote hajawa tayari kubadili mtindo wake wa uchezaji , jana angeweza kuwa mtu muhimu sana kwa Simba kwa upande wake kwa kuwa ni mtu mwenye kipaji na mwenye uwezo mkubwa ila hatumii maarifa kusaidia kipaji chake , ni dhahiri kocha Moses Basena alikuwa na malengo na kumuweka benchi akilenga kumtumia kama Super-sub pale ambapo mpinzani anapokuwa amechona kwa jinsi alivyo na uwezo wa kumiliki mipira , kupiga chenga, kasi na uwezo wake wa kupiga krosi hatari lakini alimuangusha kocha sana kwa kuwa alipoingia alionekana kama yeye ndio alikuwa amechoka na Nsajigwa alikuwa ameingia kwa kuwa alikuwa anamkabili na kummudu kwa urahisi sana . ( 3/10 )

Salum kanoni .
Salum Kanoni aliingia huku kocha akiwa na mawazo ya penati kwa sababu kanoni ni moja kati ya wapiga penati wazuri ambao simba inao ila haikuwa hivyo kwa kuwa aliingia na Simba ikafungwa hivyo alihitajika kuiokoa timu yake , hakuwa makini kwa yale aliyokuwa akiyafanya , alipata nafasi mbili za kupiga mashuti lakini hakuwa makini na aliishia kupaisha jukwaani . (-)

Kocha Moses Basena.
Mpaka sasa bado ni mapema nab ado anahitaji muda wa kuingiza falsafa yake kwenye timu japo bado anaonekana kuwa si mkali kwa wachezaji wake ambao hawana umakini na bado hawana ari ya upiganajni ambayo iko kwa wenzao Yanga , bado hatujaona mkono wake kwenye usajili ila anahukumiwa kwa usajili wa Derick Waluhya ambaye anaonekana kusajiliwa kwa kukurupuka mno .

Sunday, July 10, 2011

YANGA WAMKUMBUKA PEPE KALE

huyu ni shabiki wa yanga akiwa na bango la kumkumbuka mwanamuziki PEPE KALE, baada ya yanga kuchukua ubingwa wa kagame mwaka 1993 jijini kampala PEPE KALLE ALIWATUNGIA YANGA WIMBO WA KUWAPONGEZA..



YANGA YATWAA UCHAMPIONI WA KAGAME CASTLE CUP 2011 KWA KUIFUNGA SIMBA BAO 1-0







HAWA NI MASHABIKI WA SIMBA WALIVYOMIMINIKA KIWANJANI KUIPA SUPPORT TIMU YAO..







HUU NI UPANDE WA MASHABIKI WA YANGA.....






HAPA NIKIWA NA MWEUSI MWENZANGU JB ( SHABIKI WA MNYAMA ) MUIGIZAJI MAARUFU WA SINEMA ZA KIBONGO





MASHABIKI WA NAMNA HII HAWAPO SANTIAGO BERNARBEU PEKE YAKE,HATA BONGO WAPO PIA..






HUYU NI JAMHURI KIWHELU ALIYEIONGOZA SIMBA KUTWAA KOMBE HILI MWAKA 1991 KWENYE UWANJA WA ZAMANI WA TAIFA KWA KUIFUNGA SC VILLA MABAO 3-0,HUKU YEYE AKIIBUKA 'MAN OF THE MATCH' BAADA YA KUMFICHA ALIYEKUA MSHAMBULIAJI HATARI WA VILLA WAKATI HUO MAJJID MUSISI.






KASSIM DEWJI NAYE ALIKUEPO KUIPA SUPPORT SIMBA..











MUDDY SEBENE( WAPILI KUTOKA KUSHOTO), MASANJA WA ORIJINO KOMEDI (KATIKATI ) PAMOJA NA 'KIWADINHO'( WAPILI KUTOKA KULIA ) NA WADAU WENGINE PIA WALIKUEPO..






YUSUF MANJI (KATIKATI) NAYE ALIKUEPO KUISHUHUDIA TIMU YAKE YA YANGA.





RIDHIWANI KIKWETE ( KUSHOTO ) NI SHABIKI MKUBWA WA YANGA NAYE PIA ALIKUEPO KUIPA SUPPORT TIMU YAKE..










MAKAMU MWENYEKITI WA SIMBA GEOFREY NYANGE ' KABURU ' AKISEMA MAMBO YOTE DOLE,HII ILIKUA NI BAADA YA MCHEZO KUMALIZIKA...






BAADHI YA WADAU WA SIMBA WAKIWA HAWAAMINI KAMA MCHEZO UMEMALIZIKA KWA TIMU YAO KUPOKEA KIPIGO CHA BAO MOJA KWA SIFURI..






HAPA ILIKUA KABLA YA UMEME KUKATIKA...











WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA SIMBA MZEE KINESI ( MWENYE MVI ) PAMOJA NA IBRAHIM MASOUD 'MAESTRO ' ( ALIYESHIKA TAMA NA AMEVAA JEZI NYEKUNDU ) WAKIWA HAWAAMINI KAMA KWELI TIMU YAO IMEFUNGWA NA YANGA..





HAPA MCHEZO ULIKUA UNAELEKEA UKINGONI HUKU SIMBA IKIWA NYUMA YA BAO 1-0, MASHABIKI WA TIMU HIYO KAMA VILE HAWATAKI KUAMINI KINACHOTOKEA...





WAZIRI WA HABARI,VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO EMANUEL NCHIMBI AKIWA AMEVALIA SHATI LENYE RANGI NYEKUNDU NA NJANO, HII NI KUONYESHA ALIKUWA HAJAFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE...





MWENYEKITI WA YANGA LLOYD NCHUNGA ( KOTI JEUSI NA SHATI YA KIJANI ),KUSHOTO KWAKE NI ALIYEKUWA MWENYEKITI KABLA YAKE BWANA IMAN MADEGA WAKISHANGILIA MARA BAADA YA FILIMBI YA MWISHO KUPULIZWA NA KUASHIRIA YANGA KUIBUKA MABINGWA WA KAGAME CASTLE CUP 2011.





GOLIKIPA WA YANGA SHABANI KADO AKIMFANYIA MAHOJIANO NAHODHA WAKE SHADRACK NSAJIGWA....





GOLIKIPA WA YANGA YAW BERKO AKIMSHKURU MUNGU MARA BAADA YA MCHEZO KUMALIZIKA..




MUUAJI KENETH ASAMOAH....KIKUBWA NI KUWA MVUMILIVU NA PIA KUJITUMA SANA MAZOEZINI...PIA HILI BAO LANGU LA LEO NALI-DEDICATE KWA MASHABIKI WOOTE WA YANGA POPOTE PALE WALIPO....





BEKI MAJERUHI WA YANGA STEFANO MWASIKA ( MWENYE SUTI ) AKIWA NA MMOJA WA VIONGOZI WA KAMATI YA USAJILI YA YANGA BWANA SEIF.






HUYU NI CHIDI GUMBO ALIYETOA PASI YA GOLI LA YANGA......MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI...






ALAMBAAAA....ALAMBAAAAA...ALAMBAAAAAA ....ALAMBAAAA
NDIVYO INAVYOELEKEA HAPA MZEE YUSUF AKIWAONGOZA WACHEZAJI NA MASHABIKI WA YANGA KUIMBA HICHO KIBAO CHAKE MAARUFU CHA TAARAB..




HUYU NI MZEE YUSUF (MMILIKI NA MUIMBAJI WA BENDI YA JAHAZI MODERN TAARAB ) MMOJA WA WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI YA YANGA PIA ALIKUEPO..









HAPA NI WAKATI UMEME ULIPOKATIKA UWANJANI....KULIKUA KAMA HIVI...GIZA TOTORO..







HATIMAYE YANGA WAKAKABIDHIWA NDOO GIZANI....
















NAHODHA WA YANGA SHADRACK NSAJIGWA AKINYANYUA JUU UBINGWA WA KAGAME CASTLE CUP 2011...

BEND IT IN LIKE DAVID BECKHAM

COUNTDOWN SIMBA VS YANGA :BINGWA ATAAMULIWA NA MATUTA..

Hatimaye matarajio ya watanzania wengi yametimia kwani michuano ya Kagame Castle Cup inafikia tamati kwa mchezo wa fainali unaowakutanisha wenyeji Simba na Yanga . Kama ungemuuliza shabiki yoyote wa vilabu hivi nani angetwaa uchampioni wa michuano hii mwanzoni ni dhahiri angekwambia kuwa timu yake itashinda hivyo njia pekee ya kumaliza ubishi huu ilikuwa kukutana kwenye mchezo wa fainali anayeshinda ashinde na anayefungwa angoje siku nyingine .
Ukitazama timu hizi mbili kila moja ina sehemu yake ambayo inaipa kiburi na uhakika wa kuibuka ushindi lakini upande wa pili nao kila timu ina mapungufu yake ambayo yanaipa woga .

Besena na Falsafa ya ulinzi..
Makocha wa timu hizi mbili kidogo wamekuja na falsafa tofauti hasa kwa kocha wa Simba Moses Basena . Mganda huyu ameifanya Simba iwe na safu ya ulinzi ambayo ina uimara ambao ulikosekana msimu uliopita wa ligi ya Vodacom . Labda hii ni kwa sababu timu hii imekosa wamaliziaji huku ikiwa na viungo wengi ambao wanapenda kuuchezea mpira hali inayoweza kuwagharimu wanapokutana na timu inayolinda kwa nidhamu ya hali ya juu na ndio maana hadi michuano hii inafikia hatua ya fainali Simba imeruhusu wavu wake kuguswa mara mbili tu . Hivyo nadhani ni sahihi kusema kuwa Basena ana falsafa ambayo inazingatia zaidi ulinzi.

Sam Timbe Kuimalisha kiungo…
Kwa upande wa Jangwani mganda mwingine Sam Timbe anaonekana kuwa mtu ambaye anapenda timu yake ishambulie mwanzo mwisho huku ikiwatumia walinzi wanaotumia nguvu sana wakati wanapokabiliana na washambuliaji toka timu pinzani , labda ni kwa sababu ya aina ya uchezaji wa walinzi alio nao ambao ni watu “physical” kina Fusso,Cannavaro,Taita na Oscar Joshua. Timbe anaonekana kuwa ameibadilisha Yanga kwa kiasi kikubwa kwenye safu ya kiungo ambayo inaongozwa na Rashidi Gumbo mchezaji aliyesajiliwa toka Simba akishirikiana na kiungo mwingine Nurdin Bakari ambaye naye alitoka Simba muda mrefu kidogo uliopita .Watu hawa wameonekana sana kuelewana kwenye safu ya kiungo tofauti na ilivyo falsafa halisi ya Yanga ambayo kihistoria hupenda kuwatumia zaidi mawinga kama kina Ngassa, Nsa Job , Edibily Lunyamila na wengine wengi waliopita siku za nyuma japo hawajaitupilia mbali falsafa hii kwani wapo Julius Mrope na Kiggi Makasi . Safu ya Ushambuliaji ya Yanga ndio inayoonekana kuwa na uhai zaidi unapopambanua safu mbili za ushambuliaji za Simba na Yanga . Hadi kufikia fainali Yanga imetupia wavunia mabao saba kwenye hatua ya makundi na kwenye mechi za mtoano walishindwa kufunga bao hata moja na kupita kwa njia ya matuta. Simba wao wamefunga mabao sita hadi kufikia hatua hii.
Simba kutokua na mshambuliaji asilia…
Ukitazama vikosi vya timu zote mbili Yanga wanaonekana kuwa kamili kuliko Simba kwani wanaonekana kuwa na “first eleven” inayoeleweka na ambayo inaweza kujenga “chemistry” yaani maelewano tofauti na Simba ambao kikosi chao sio kile kile na kimekuwa kikibadilika badilika sana karibu kila mechi . Unaweza kukuta leo Banka anacheza nafasi ya namba tisa , kesho akacheza kumi na mwenendo ndio umekuwa huo karibu kila mechi .
Hili linaweza kuwa na hasara au faida kwa sababu wakati mwingine mpinzani anaweza kukosa mbinu ya kukabili kwa sababu tu ameshindwa kujua ni timu ipi itakayoingia siku hiyo na hasara yake ni pale ambapo timu yako haina “chemistry” kitu ambacho Yanga wanaonekana kuwa nacho .Simba tangu mchezo wa kwanza dhidi ya Vital O wamegharimiwa na tatizo moja kubwa ambalo ni kukosa wamaliziaji , hili limesababisha wekundu kukosa mabao mengi sana ya wazi . Ukitazama mfumo ambao wanaingia nao ambao huwa unabadilika badilika hata mchezoni Simba wamekuwa wakiwatumia mabeki wane , viungo wanne na washambuliaji (viungo wanaolazimika kucheza kama washambuliaji) wawili wanaocheza mmoja mbele mmoja nyuma katika mfumo wa 4-4-1-1 na wakati mwingine wanacheza 4-4-2 diamond huku kiungo mmoja akisimama mbela ya mabeki na mwingine nyuma ya washambuliaji na hata wakati mwingine wamekuwa wakicheza 4-1-3-2 au 4-1-3-1-1 ambapo mara nyingi unakuta kaseja anasimama langoni chollo akisimama kulia , amir maftah akisimama kushoto na wawili kati ya Waluhya Derick,Kevin Yondani na Juma Nyoso wakisimama kati na kuna wakati Derick waluhya alisimama pembeni kulia jambo ambalo almanusra liwaletee Simba balaa na kwenye safu ya kiungo Jerry Santo amekuwa akisimama kama namba sita kwenye nafasi ya holding au combat midfielder akiwa mchezaji pekee kwenye safu hiyo aliyecheza kwa “consistency” ya hali ya juu huku pembeni kulia akicheza wakati mwingine Salum Machaku na wakati mwingine Ulimboka na Musa Hassan Mgosi amekuwa akicheza kama kiungo anayetokea upande wa kushoto na Shija Mkina amekuwa akiingia tokea benchi la wachezaji wa akiba kujaza nafasi ya winga ya kulia . Safu ya viungo wa Simba imejaa watu ambao wanajua kuuchezaea mpira kwa ufundi wa hali ya juu na wanapiga pasi nyingi sana nzuri ila shida kubwa imekuwa kwenye umaliziaji ambako Mohamed Banka na Haruna Moshi wamekuwa wakipangwa kama washambuliaji. Watu hawa wawili kiasili ni viungo ambao wanacheza namba nane au kama wakicheza ushambuliaji wanacheza namba kumi nyuma ya mshambuliaji .Sasa wanapocheza kama washambuliaji Simba inakosa mabao mengi sana kwa kuwa hawa watu si wafungaji ufundi wao wote unaishia kwenye pasi za mwisho na sio kuzipasia nyavu .




Mfumo wa Yanga ni 4:4:2 na 4:4:1:1
Kwa upande wa Yanga wamekuwa wakitumia mfumo wa 4-4-2 au 4-4-1-1 yaani mabeki wakiwa kwenye mstari mmoja , viungo kwenye mstari mmoja na washambuliaji wawili moja nyuma ya mwingine . Godfrey Taita,Shadrack Nsajigwa , Oscar Joshua , Chacha Marwa na Nadir Haroub Canavaro wamekuwa wakisimama kwenye mstari wa walinzi wa Yanga na kati ya hawa Chacha Marwa ameonekana kuwa “outstanding ” kuliko wenzie kwa jinsi anavyocheza kwa ujasiri akikabiliana na washambuliaji kwenye zile “one-to-one situation” . Kwa walinzi wa Yanga shida imekuwa moja nayo ni kutumia nguvu nyingi kuliko maarifa na wakati mwingine wanapokutana na washambuliaji wanaocheza ‘begani’ mwa beki wamekuwa wakichanganyikiwa kama ilivyotokea kwa Jonas Sakuwaha wa AL Mareikh na Owen Kasule wa Bunamwaya ambapo mara zote hizo Yanga walijikuta wakiruhusu mabao ya kizembe . Viungo wa yanga wamekuwa wakicheza vyema , Nurdin Bakari amekuwa aki-link vyema na Rashid Gumbo na Julius Mrope kwa upande wake amekuwa akiwapa wakati mgumu sana mabeki kwa kasi yake na chenga , Kiggi Makasi yeye ameonekana kuwa na homa za vipindi kwani kuna wakati anakuwa hayuko mcchezoni ana anakuwa anaipa timu yake wakati mgumu kwani inakuwa kama inacheza pungufu japo mipira yake anayoileta toka upande wa kushoto ina madhara sana .
Washambuliaji wa Yanga ndio wamekuwa gumzo haswa Hamis Kiiza na Davis Mwape japo jinsi wanavyotumiwa kidogo inatia mashaka . Davis Mwape amekuwa akilazimika kucheza nyuma ya mshambuliaji mwingine jambo ambalo kwa mwili wake mkubwa linamshinda kwa sababu anashindwa kupima dribbling zake , kuna wakati ambapo anashindwa kupiga mahesabu ya wakati gani wa kuusogeza mpira na wakati gani wa kuupiga , kama angekuwa kiungo hili lisingempa shida ila kwa kuwa yeye ni aina ya wachezaji tunaowaita “18 yard players” yaani mchezaji wa kwenye eneo la 18 tu na nje ya hapo si mahala kwake . Pamoja na hayo ameweza kufunga mabao mawili ambapo mojawapo alilofunga dhidi ya Bunamwaya lilikuwa bao muhimu kwani liipa Yanga ushindi ambao uliwahakikishia uongozi wa kundi . Hamis Kiiza kwa upande wake ameonyesha umahiri wake kwenye ufungaji na kama Simba hawatampa ulinzi wa kutosha hakika atawaliza .
Kukosekana kwa Boban na Santo

Tatizo moja ambalo Simba watakuwa nalo kwenye mchezo wa fainali dhidi ya watani wao ni kuwakosa Haruna Moshi na Jerry Santo ambao wana kadi mbili zilizofuatana . Wote walipata kadi za njano kwenye mechi ya Robo fainali dhidi ya Bunamwaya na wakapata teka kadi kama hiyo dhidi ya Al Mareikh kwenye nusu . Kati ya hawa Simba watamkosa sana Jerry Santo mtu ambaye ukimuacha Juma Kaseja kama Simba wakitwaa ubingwa huu basi anaweza kuwa mchezaji wao wa michuano . Santo ni mtu anayetambua majukumu yake na anayatimiza kwa asilimia zote . Kukosekana kwa Boban kunaweza kusiwe pengo kubwa kwa sababu wapo watu ambao wanaweza kujaza nafasi yake vyema . Kumkosa Santo kunaweza kumaanisha kuwa Basena akalazimika kumtumia mtu kama Waluhya kama jeraha lake litapona katika nafasi ya kiungo wa chini au Patrick Mafisango japo Mafisango ni mzuri sana kwa kiungo cha juu .Kwa upande wa Kevin Yondani na Juma Nyoso watakuwepo japo Derick Waluhya kama atapona atakuwa na umuhimu wake kwa jinsi alivyo na uwezo mkubwa wa kuusoma mchezo kuwaliko wenzie anaopigania nao nafasi ya beki wa kati, Ulimboka mwakingwe ameonyesha kiwangi kizuri katika mechi zake zote alizocheza na uzoefu wake wa mechi kama hii unampa faida ya ziada ya kupewa nafasi . Kama kanuni ziotaruhusu na kama Simba walisajili mapema jina la Mwinyi kazimoto na kama atapangwa atakuwa na umuhimu kwa jinsi anavyojua jukumu la “playmaker” na anaweza kuwa na mchango mkubwa sana.
Yanga na kikosi kamili..
Yanga wanaingia wakiwa na kikosi kizima ambacho hakina mapungufu yoyote . Golini akiwepo Yaw Berko ambaye ukiacha kungushwa na mabeki wake ni “reliable” sana golini , Nsajigwa , Taita , Canavarro na Chacha Marwa ni watu ambao wameonyesha uwezo wakiwa kwenye nafasi ya Ulinzi na hakuna sababu ya kutowapanga kwenye fainali , Gumbo na Nurdin moja kwa moja wana nafasi zao kwenye kikosi cha kwanza kama ilivyo kwa maforward wawili Mwape na Kiiza japo rekodi inaweza kumfanya Timbe alazimike kumtumia Jerryson Tegete kwani amekuwa akiwafunga Simba mara kwa mara na uwepo wake uwanjani unawafanya walinzi wa Simba na kipa wao kuwa roho juu.
Sam Timbe
vs Moses Basena..
Makocha wa timu zote mbili wana historian a Michuano hii . Sam Timbe amewahi kutwaa ubingwa mara tatu akiwa na timu tatu tofauti . Labda historia itampendelea tena na kumpa ubingwa wan ne na wa kihistoria . Bassena amewahi kucheza fainali mara moja ambapo alipoteza kwa Tusker Fc iliyokuwa inaongozwa na nahodha Jerry Santo katika mwaka ambao Yanga ilimkimbia mnyama kwenye mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu . je ataendelea na historia yake ya kuwasindikiza wenzie ?
Ukitazama historia ya vilabu hivi viwili kwenye michuano hii unapata sababu ya ziada ya kununua tiketi mapema na kuwahi kuingia uwanjani . Timu hizi zimewahi kukutana mara mbili ambapo kila mmoja ameshinda mara moja na atakeyeshinda safari hii atakuwa mbele ya mwenzie .
Itakuwa fainali ngumu sana kwa sababu timu hizi zina historia ambayo iko mbali zaidi ya michuano hii na kwa kila mmoja kumfunga mwenzie kwa njia yoyote ile ni jambo la thamani kubwa sana na mchezo huu unaongezewa utamu na ukweli kuwa ni mchezo wa fainali ambao lazima mshindi apatikane. Je itakuwa kijani na njano au nyekundu na nyeupe ambao wataitawala Afrika mashariki na kati? Jibu litapatikana baada ya dakika tisini au 120 au baada ya mikwaju ya penati iwe mitano au ile ya piga ni kupige hadi mtu afe .

prediction:Mshindi atapatiana baada ya dakika 90.

COUNTDOWN KAGAME CASTLE CUP FINAL: SIMBA vs YANGA.


MASHABIKI wa soka nchini hawakuwa na imani kabisa na timu zao, Simba na Yanga kama zinaweza kufika hata Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Castle, kutokana na sababu tatu kubwa, ambazo ni; kukurupushwa kuingia kwenye michunao hiyo, maandalizi duni na pia kushuka kwa viwango vya timu zetu katika miaka ya karibuni.
Lakini hali imekuwa tofauti, miamba hiyo ya soka ya Tanzania miaka nenda, rudi leo inakutana kwenye fainali ya michuano hiyo, baada ya kufanya kazi ngumu kuanzia mechi za makundi hadi Robo Fainali na Nusu Fainali.
Simba iliyokuwa Kundi A, ilifuzu kama kinara wa kundi hilo, baada ya kujikusanyia pointi nane kutokana kushinda mechi mbili na kutoka sare mbili, utamu zaidi kipa Juma Kaseja akiweka rekodi ya kuwa mlinda mlango pekee ambaye hakuruhusu nyavu zake kutikiswa hata mara moja katika hatua ya makundi.
Simba ikakutana na mabingwa wa Uganda, Bunamwaya FC katika Robo Fainali na wakafanikiwa kushinda mabao 2-1, shukrani kwake kiungo Mkenya, Jerry Santo Evans aliyefunga bao la ushindi dakika ya 84, katika mchezo ambao dhahiri ulikuwa mgumu kwa Wekundu wa Msimbazi.
Baada ya hapo, Simba ikakutana na timu ngumu, tena sana kulingana na timu zote zilizokuwa kwenye michuano hii, El Merreikh ya Sudan, wengi miongoni mwa wachambuzi wa soka wakiipa timu hiyo kura chache mno za kukata tiketi ya kucheza mechi ya mwisho.
Mchezo ulianza vibaya kwa Simba, wakitanguliwa kufungwa bao na mabingwa wa Sudan, dakika ya 12 mfungaji akiwa ni Adiko Rime, kabla ya mshambuliaji mkongwe Ulimboka Alfred Mwakingwe kuisawazishia timu hiyo bao tamu kwa kichwa cha mkizi, dakika ya 24.
Dakika 90 zilitimu matokeo yakiwa 1-1 na dakika 30 za nyongeza pia hazikubadilisha matokeo na ndipo mchezo ulipohamia kwenye mikwaju ya penalti, Simba ikashinda 6-5, shujaa wa michomo hiyo Juma Kaseja akicheza penalti ya Mzambia Jonas Sakuwaha.
Sasa Simba leo watamenyana na watani wao wa jadi, Yanga katika fainali, hii ikiwa ni mara ya tatu kihistoria timu hiyo kukutana katika hatua hiyo ya michuano hii, kwanza mwaka 1975 na pili mwaka 1992, mechi zote zikipigwa visiwani Zanzibar na kila timu ilishinda mechi moja.
Mabao ya Sunday Manara na Gibson Sembuli (sasa marehemu) mwaka 1975 yaliipa Yanga ushindi wa 2-0 dhidi ya Simba waliokuwa mabingwa watetezi na kutwaa taji hilo kwa mara ya kwanza- wakati ushujaa wa kipa Mwameja Mohamed kupangua mikwaju ya penalti uliipa Simba ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa tena taji hilo.
Kwa Dar es Salaam Simba na Yanga hazijawahi kukutana kwenye michuano ya Kagame, ingawa mwaka 2008 zilipaswa kumenyana katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu, lakini Watoto wa Jangwani ‘wakapotea’ njia ya kuelekea ulipo Uwanja wa Taifa, na Wekundu wa Msimbazi wakapewa ushindi wa mezani.

SIMBA ILIVYOTWAA MATAJI SITA YA AWALI:
Simba ndio bingwa wa kihistoria wa michuano hii, ikiwa imetwaa taji hilo mara sita, ikifuatiwa na AFC Leopards na Tusker za Kenya, ambazo zote zimetwaa taji hilo mara tano kila moja, wakati Yanga sawa na APR FC ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya, SC Villa ya Uganda zimetwaa mara tatu kila moja taji hilo.
Luo Union, El-Merreikh zimechukua mara mbili kila moja, ATRACO, Rayon Sport za Rwanda, KCC na Polisi FC za Uganda kila moja imetwaa mara moja.

ZANZIBAR MWAKA 2002:
Michuano ya mwaka huo, ilianza Februari 16, ikishirikisha timu za Prince Louis ya Burundi, Mebrat Hail ya Ethiopia, Oserian Fastac, Tusker FC za Kenya, waliokuwa mabingwa watetezi, APR ya Rwanda, Elman ya Somalia, Simba SC, SC Villa na wenyeji Forodha na Mlandege za Zanzibar.
Simba ilipangwa Kundi B pamoja na Tusker, Forodha, Prince Louis na Elman na mechi ya kwanza Februari 8, ililazimishwa sare ya bila kufungana na Elman, kabla ya Februari 21 kutoka nyuma kwa bao 1-0 lililofungwa na Seleman Nsabah dakika ya 14 na kuifunga 2-1 Prince Louis, Emmanuel Gabriel akisawazisha dakika ya 27 kabla ya Yussuf Macho ‘Musso’ kufunga la pili dakika ya 78.
Febaruari 23 katika mchezo wa tatu, Simba iliitandika Forodha mabao 3-1, Joseph Kaniki akitangulia kufunga dakika ya 22, Steven Mapunda ‘Garrincha’ akifunga la pili dakika ya 65 na Macho kupiga la tatu dakika ya 90 na Februari 25, Wekundu hao wa Msimbazi walihitimisha mechi zao za Kundi B kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya 1-0, waliojifunga wenyewe dakika ya 88, Kevin Malumbe akimfunga kipa wake katika harakati za kuokoa.
Kwa matokeo hayo, Simba iliongoza Kundi hilo kwa pointi zake 10, na kwenye Nusu Fainali Machi Mosi, iliifunga Mlandege mabao 2-0, wafungaji
Macho dakika ya 37 na Sheikhan Rashid kwa penalti dakika ya 90, kabla ya kuifunga Prince Louis Machi 3 kwenye fainali, bao pekee la Nteze John Lungu dakika ya suita ya mchezo.
Siku hiyo, kikosi cha Simba SC kilikuwa; Mohamed Mwameja, Said Sued, Ramadhani Wasso/ Majuto Komu dk 35, Amri Said, Boniface Pawasa, Suleiman Matola, Stephen Mapunda/Joseph Kaniki dk 74, Shekhan Rashid, Yusuf Macho, Nteze John/Emmanuel Gabriel dk 61 na Mark Sirengo.

DAR ES SALAAM MWAKA 1996:
Michuano ya mwaka huo, Simba ikiwa bingwa mtetezi ilipangwa Kundi A pamoja na Al Hilal ya Sudan, APR ya Rwanda na Small Simba ya Zanzibar.
Ilianza kwa kuifunga 2-0 Small Simba, kabla ya kufungwa 1-0 na APR na baadaye kuibwaga 1-0 Al Hilal.
Simba ikafuzu kuingia Nusu Fainali kama mshindi wa pili wa Kundi hilo,na kukutana na Gor Mahia ya Kenya na kufanikiwa kushinda 1-0, bao pekee la Bitta John.
Katika fainali, Simba ilikutana na APR na bao pekee la beki mahiri enzi hizo George Magere Masatu dakika ya 115, baada ya kutimu dakika 90 bila timu kufungana, liliipa Simba ubingwa wa tano wa michuano hiyo.

DAR ES SALAAM MWAKA 1995:
Michuano ya mwaka huo pia ilifanyika Dar es Salaam na Simba walipangwa Kundi A tena pamoja na Express ya Uganda, Morris Supplies ya Somalia na Adulis ya Somalia.
Katika mchezo wa kwanza ililazimishwa sare ya kufungana 1-1 na Express, kabla ya kuifunga Morris Supplies 3-1 na Adulis 4-1, hivyo kuongoza Kundi hilo kwa kufikisha pointi saba na kutinga Nusu Fainali, ambako ilikutana na El Mourada ya Sudan Februari 9 na kushinda 1-0, hivyo kujikatia tiketi ya fainali.
Ilikutana na Express ya Uganda katika fainali na dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Hussein Amaan Marsha akitangulia kuwafungia waganda katika harakati za kuokoa dakika ya 51, lakini swahiba wake George Masatu akasawazisha dakika ya 53.
Dakika 120 zikamalizika timu hizo zikiwa zimefungana 1-1 na ndipo kwa mara nyingine, umahiri wa kipa Mwameja Mohamed ukainufaisha Simba kwenye mikwaju ya penalti na ikashinda 5-3.

ZANZIBAR MWAKA 1992:
Wakiwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, walikutana na watani wao wa jadi, Yanga katika fainali.
Kwa kuwa mwaka 1975 Yanga iliifunga Simba mabao 2-0 visiwani Zanzibar, wengi waliamini historia itajirudia na mwaka 1992, ila mambo yakawa tofauti.
Ikitokea Kundi A, Simba ilizipiga Bata Bullets ya Malawi na Small Simba ya Zanzibar na kutinga Nusu Fainali, ambako iliifunga Rivatex Eldoret ya Kenya mabao 2-0.
Katika fainali, dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 na mchezo kuhamia kwenye mikwaju ya penalti na kwa mara nyingine kipa wa zamani wa Reading ya England, Mwameja Mohamed akaonyesha umahiri wake kwa kucheza penalti ya Abubakar Salum ‘Sure Boy’ na baadaye ya David Mwakalebela hivyo kuipa Simba ubingwa wa mwaka huo.

DAR ES SALAAM MWAKA 1991:
Kombe hilo halikuwahi kukanyaga tena Tanzania, tangu Yanga waende kuliacha Kenya mwaka 1976 na michuano ya mwaka 1991 ilikuwa mkombozi wa taifa letu.
Ikishirikisha timu za Gor Mahia ya Kenya, Limbe Leaf Wanderers ya Malawi,
El-Maorada ya Sudan, SC Villa ya Uganda na wenyeji Simba SC na Coastal Union ya Tanga, ilifanyika katika vituo vya Dar es Salaam na Tanga.
Simba iliongoza Kundi A mjini Dar es Salaam na kutinga Nusu Fainali ambako iliifunga Gor Mahia na kukata tiketi ya kuingia fainali ilipokutana na SC Villa ambako ilishinda mabao 3-0, wafungaji Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’ aliyefunga mawili na Hassan Afif moja.
Katika mchezo huo, kikosi cha Simba kilichorejesha Kombe hilo nchini kilikuwa; Iddi Pazi, Raphael Paul, Twaha Hamidu, Jamhuri Kihwelo ‘Mrema’, Method Mogella (sasa marehemu), Iddi Suleiman ‘Meya’, Issa Kihange, Bakari Iddi, Ayoub Mzee/Hassan Afif, Zamoyoni Mogella na Itutu Kigi ‘Road Master’.
Ambao hawakushirikii mechi hiyo walikuwa ni Mackenzie Ramadhan, Khalfan Ngassa, Gebo Peter, Hasan Banda, Mavumbi Omar, Hamisi Gaga, Frank Kasanga Bwalya.
Mambo mawili ya kukumbukwa kwenye michuano hii; kipa Iddi Pazi ‘Father’ alicheza mechi zote za Simba bila kuruhusu bao hata moja, lakini pia kocha Abdallah Kibadeni ‘King’ alimfukuza beki tegemeo wa timu hiyo wakati huo Frank Kasanga ‘Bwalya’ kwa utovu wa nidhamu na akaamua kumtumia kama sentahafu kiungo Method Mogella badala ya kiungo.

DAR ES SALAAM MWAKA 1974:
Hii ilikuwa michuano ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kufanyika na ilichezwa kwa mtindo wa Ligi mjini Dar es Salaam ikishirikisha timu za Simba SC, Navy FC ya Zanzibar, Simba ya Uganda na Abaluhya FC ya Kenya.
Simba ilianza kwa sare ya 2-2 na Navy FC, kabla ya kuifunga Abaluhya FC 1-0 na badaaye kutoka sare ya bila kufungana na Polisi Uganda.
Kwa matokeo hayo, Simba ikachukua ubingwa kwa kufikisha pointi tano, ikifuatiwa na Abaluhya iliyofikisha pointi tatu, Navy pointi mbili sawa na Simba ya Uganda.
Hivyo ndivyo Simba ilivyotwaa mataji yake sita, vipi kwa watani wao wa jadi, Yanga walichukuaje mataji yao matatu?





YANGA ILIVYOTWAA MATAJI MATATU YA AWALI:
Yanga iliyokuwa Kundi B la michuano ya mwaka huu, ilifuzu kama kinara wa kundi baada ya kujikusanyia pointi saba kutokana na kushinda mechi mbili na kutoka sare moja.
Katika Robo Fainali, Yanga ilikutana na Red Sea ya Eritrea na kushinda kwa penalti 6-5, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 za mchezo huo.
Katika Nusu Fainali, Yanga ilikutana na St George ya Ethiopia na kushinda tena kwa penalti 5-4, kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 120. Sasa leo inacheza fainali na watani wao wa jadi, Simba SC, hii ikiwa ni mara ya tatu kwao kukutana kwenye fainali ya michuano hiyo. Yanga tayari ina mataji ya michuano hiyo na leo inasaka la nne, je hayo matatu ilichukuaje?

ZANZIBAR MWAKA 1975:
Iliingia kama bingwa wa Tanzania baada ya kuifunga Simba SC katika fainali ya Ligi mwaka 1974 Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, wakati watani wao hao waliingia kama mabingwa watetezi wa michuano.
Yanga ilipangwa Kundi B pamoja na Express ya Uganda na Mufulira Wanderers ya Zambia. Yanga ilianza kwa kuifunga Express FC mabao 4-0 na baadaye kutoka sare ya 1-1 na Mufulira, hivyo kuongoza Kundi hilo na kukata tiketi ya kuingia Nusu Fainali.
Katika Nusu Fainali, Yanga iliifunga Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 na kukata tiketi ya kuingia fainali Janauri 13, mwaka huo ilipokutana na watani wao wa jadi, Simba SC.
Mabao ya Sunday Manara ‘Computer’ na Sembuli yaliipa Yanga ushindi wa 2-0 na taji la kwanza la michuano hiyo.

KAMPALA, UGANDA MWAKA 1993:
Ilikwenda kama bingwa wa Bara na watano wao, Simba walikwenda kama watetezi wa taji na huko Yanga walipangwa Kundi A pamoja na wenyeji SC Villa na Malindi ya Zanzibar.
Katika mchezo wa kwanza, Yanga ilifungwa 3-1 na Villa, siku hiyo kabla ya kuibuka na kuifunga Malindi mabao 2-1, yote yakitiwa kimiani na Said Nassor Mwamba ‘Kizota’, sasa marehemu, hivyo kukata tiketi ya kuingia Nusu Fainali.
Katika Nusu Fainali, Yanga ilikutana na Express FC na kushinda mabao 3-1, hivyo kutinga fainali ambako ilikutana tena na SC Villa.
Kwa kuzingatia matokeo ya mchezo wa awali kwenye Kundi A, Yanga haikupewa nafasi kabisa ya kufurukuta mbele ya SC Villa, lakini mambo yalikuwa tofauti, mabao ya Said Mwamba na Edibily Lunyamila, yaliipa timu hiyo ushindi wa 2-1 pamoja na taji la pili la michuano hiyo.
Marehemu Kizota aliibuka mfungaji bora wa michuano hiyo.

KAMPALA, UGANDA MWAKA 1999:
Ilikwenda kama bingwa wa Bara, ikiwa mwakilishi pekee na ilitua huko, huku mashabiki wengi wa soka Uganda wakiwa na kumbukumbu ya kile kilichofanywa na klabu hiyo mwaka 1993.
Timu zilizoshiriki michuano hiyo ni Vital'O ya Burundi, Mebrat Hail ya Ethiopia, AFC Leopards ya Kenya, Kiyovu Sport, Rayon Sport za Rwanda,
Naadiga Dekedaha ya Somalia, KMKM ya Zanzibar, Al Hilal ya Sudan, Yanga, wenyeji Express na SC Villa za Uganda wakati Red Sea ya Eritrea ilijitoa dakika za mwishoni.
Kwa matokeo hayo, Kundi D ilimokuwa Yanga lilibakiwa na timu mbili tu, yaani mabingwa hao wa Bara na mabingwa watetezi.
Mechi ya kwanza, Yanga ilifungwa 3-0 na Rayon Januari 4 na ziliporudiana siku mbili baadaye, Yanga walilipa kisasi kwa ushindi wa 3-0 pia, mabao ya
Sekilojo Chambua dakika ya 23 na 57 na Kali Ongala dakika ya 59.
Katika Robo Fanali, Yanga ilikutana na Al Hilal Januari 10 na kushinda mabao 2-1, wafungaji Salvatory Edward dakika ya 14 na Edibily Lunyamila dakika ya 89 kwa penalti.
Katika Nusu Fainali, Yanga ilikutana na Vital’O ya Burundi Januari 13 na kushinda mabao 3-2, wafungaji Kally Ongara dakika ya 16, Bakari Malima dakika ya 78 na Said Mhando dakika ya 90.
Hivyo kwa mara ya pili, Yanga ilikutana na SC Villa kwenye fainali kukumbushia vitu vya mwaka 1993 na safari hii mambo yalikuwa mazito zaidi, kwani dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1 Lunyamila akiisawazishia Yanga dakika ya 42, baada ya Hassan Mubiru kutangulia kufunga dakika ya saba tu ya mchezo huo.
Mchezo ukahamia kwenye mikwaju ya penalti na Manyika Pater akaingia kwenye orodha ya makipa hodari wa kupangua penalti baada ya kupangua mikwaju miwili, Yanga ikishinda kwa penalti 4-1, Uwanja wa Nakivubo.
Hivyo ndivyo Yanga ilivyotwaa mataji yake matatu na leo inashuka dimbani kuwania taji la nne, je mambo yatakuwaje? Hapana shaka hilo ni jambo la kusubiri na kuona mambo yatakuwaje Uwanja wa Taifa jioni ya leo.