Search This Blog

Monday, April 7, 2014

WACHEZAJI WA PSG WAPEWA AHADI YA ZAIDI YA BILLIONI MOJA KILA MCHEZAJI ENDAPO WATAITOA CHELSEA KESHO

Wachezaji wa klabu ya PSG wamehaidiwa kiasi cha €450,000 kila mmoja endapo wataifunga au kuitoa Chelsea katika mchezo wa kesho wa robo fainali ya ligi ya mabingwa wa ulaya.
Gazeti la Le Parisien limeripoti kwamba Raisi wa PSG Nasser Al-Khelaifi ametoa ofa hiyo kuelekea mchezo wa kesho utakaopigwa katika dimba la Stamford Bridge. 
PSG tayari wapo mbele kwa ushindi wa mabao 3-1 waliopata wiki iliyopita jijini Paris.
Hatua inakuja siku chache baada ya kutoa ahadi ya €400,000 kwa kila mchezaji ikiwa tu watatetea kombe la ligue 1. 
€450,000 ni zaidi ya billioni 1 kwa fedha za madafu.

No comments:

Post a Comment