Search This Blog

Monday, April 7, 2014

UONGOZI WA COASTAL UNION WASHINDWA KUMLIPIA KADO GHARAMA ZA OPERESHENI YA KIDOLE.

Ikiwa leo ndio siku ambayo golikipa wa Coastal Union Shabani Kado alitakiwa kwenda kufanyiwa upasuaji wa kidole chake,mpaka jana mchana klabu yake ya Coastal Union ilikuwa haijakuwa tayari kumlipia ghalama za matibabu karibia shilingi milioni moja za Kitanzania.
''Kweli kesho ( leo ) ndio appointment yangu pale MOI ya kufanyiwa upasuaji lakini mpaka sasa sijui kama itawezekana kwani uongozi wa timu yangu bado haujalipia ghalama za matibabu,hayo ni maneno ya Kado alipokuwa akifanya mahojiano na mtandao huu hapo jana''
Mtandao huu unaendelea kufuatilia kama leo Kado atafanikiwa kufanyiwa upasuaji huo au la.

 Golikipa wa Coastal Union Shabani Kado akiwa amevaa Plasta Ngumu ( POP ).

 picha za X-RAY zikikionyesha kidole cha Kado kilichovunjika,

No comments:

Post a Comment