Search This Blog

Thursday, April 3, 2014

PANONE FC YA KILIMANJARO ILIVYOTANGAZWA BINGWA WA MKOA LIGI DARAJA LA TATU

Wachezaji wa timu ya Panone FC ya mkoani Kilimanjaro wakipasha misuli joto kabla ya mchezo wao wa kukamilisha ratiba dhidi ya waliokuwa mabingwa wa mkoa watetezi timu ya Machava Fc.
Wachezaji wa timu za Panone fc na Machava fc wakisalimiana kabla ya kuanza kwa mchezo wao wa kukamilisha ratiba.
Wachezaji wa Panone fc wakiomba dua kabla ya kuanza kwa mchezo.
Wachezaji wa timu ya Machava fc wakijadiliana jambo kabla ya kuanza kwa mchezo.
Waaamuzi wa mchezo huo tayari kwa kuanza pambano.
Benchi la ufundi lilikuwa Busy wakati wa mapumziko kuhakikisha vijana wanatoka na ushindi
Machava fc kwa upande wao pia waliweka mikakati ya ushindi.
Mgeni rasmi katika mpambano huo afisa michezo wa mkoa wa Kilimanjaro Anthony Ishumi akzungumza na timu zote mbili wakati wa mapumziko
Vijana wakambana kufa na kupona.
Hadi dakika 90 za mwamuzi Nathan zinamalizika ubao ulisomeka Panone fc 1 Machava fc 0.
Zikatolewa medali kwa wachezaji.
Wakatawazwa mabingwa wapya wa mkoa wa Kilimanjaro na kukabidhiwa kikombe cha Ubingwa.

Na Dixon Busagaga .

No comments:

Post a Comment