Search This Blog

Thursday, April 10, 2014

OMOG ANAWEZA KUANZISHA WASHAMBULIAJI WATATU DHIDI YA RUVU SHOOTING LEO!!

Na Baraka Mpenja, Dar Es salaam

VINARA wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wanaingia kwenye mechi muhimu leo hii dhidi ya  Ruvu Shooting katika uwanja wa Mabatini Mlandizi Mkoani Pwani.
Mechi hii ilitakiwa kuchezwa jana, lakini iliahirishwa kutokana na mvua kubwa kunyesha katika mji wa Mlandizi na kuufanya uwanja wa Mabatini kujaa maji mithiri ya bwawa.
Azam fc wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na `presha` ya kutafuta matokeo kwa jinsi yoyote ile kwasababu ushindi wa mabao 2-1 walioupata mabingwa watetezi, Young Africans jana uwanjanja wa Taifa dhidiya Kagera Sugar unawatishia amani katika mbio zao za kutwaa ubingwa.
Sasa Azam wana pointi 53 pointi moja mbele ya Yanga, lakini wao wana mchezo wa leo mkononi.
Endapo wana Lambalamba watashinda mechi hii, basi watakuwa wanahitaji pointi tatu pekee katika michezo miwili itakayosalia dhidi ya Mbeya City na JKT Ruvu.
Ushindi utawafanya Azam wafikishe pointi 56 kileleni na wakishinda mechi nyingine watafikisha pointi 59 ambazo hazitaweza kufikiwa na Yanga hata kama watashinda mechi zote.
Yanga anahitaji kutetea ubingwa wao, hivyo ni watumwa kwa Azam fc kwasababu wanahitaji kushinda mechi zote na kuwaombea dua mbaya Azam fc katika mechi zao.
Baada ya mechi ya jana, Yanga watakabiliana na JKT Oljoro mwishoni mwa wiki katika dimba la CCM Shk. Amri Abeid jijini Arusha, na kibarua chao cha mwisho ni dhidi ya Simba uwanja wa Taifa.
Mechi ya Azam fc leo hii itakuwa ngumu kutokana na mazingira ya aina tofauti.
Ruvu Shooting wanahitaji heshima mbele ya Azam fc ambao mpaka sasa hawajapoteza mchezo leo.
Hata kama Shooting hawahitaji ubingwa wala nafasi pili na tatu, watapambana kuhakikisha wanafanya vizuri na kuweka rekodi ya kumtandika kocha Joseph Marius Omog kwa mara ya kwanza tangu aanze kazi ya kuinoa klabu hiyo katika michuano ya ligi kuu.
Hata hivyo, Shooting wanatakiwa kujipanga vizuri kutokana na kikosi cha Azam fc kuwa katika morali kubwa ya kutwaa ubingwa wao.
Kama vijana wa Omog watafanikiwa kutwaa ubingwa, Azam fc wataandika historia mpya katika maisha yao ya soka, kwasababu ndio yatakuwa mafanikio makubwa zaidi kwasasa.
Kutwaa ubingwa wa kombe la Mapinduzi mara mbili zio ishu kwa Azam fc, ila ubingwa wa michuano mikubwa ya ligi kuu ndio ndoto yao pekee msimu huu.
Hawahitaji nafasi ya pili kwasababu wameshaipta zaidi ya misimu miwili, kwahiyo wao wanapambana kutafuta ubingwa tu.
Kwa mazingira haya ya Azam fc, Ruvu Shooting wanatakiwa kujipanga vizuri kuwazuia watu hawa wenye nia ya dhati kusaka pointi tatu muhimu.
Haitakuwa kazi nyepese kukabilina na kikosi cha Azam fc chenye mchangayiko wa wachezaji wenye uzoefu na wakongwe.
Japokuwa watakosa hudumza za Sami Haji Nuhu, Bryson Raphael, Joseph Kimwaga na baadhi ya wachezaji wengine wenye majeruhi ya muda mrefu, bado Azam wana wachezaji wengine wanaoweza kuamua matokeo siku ya leo.
Mlinda mlango Chipukiza Aishi Manula anaweza kuanza leo hii langoni, huku beki wa kulia akisimama mkongwe Erasto Nyoni.
Beki wa kushoto bila shaka atasimama bwana mdogo Gadiel Michael, beki namba nne David Mwantika huku kitasa akila Agrey Moris.
Omog anaweza kumuanzisha Michael Bolou katika nafasi ya kiungo wa Ulinzi, wakati winga wa kulia Himid Mao anaweza kuanza.
Namba 8 kwa asilimia zote Salum Abubakar ataanza kwasababu hana mpinzani katika kikosi hicho, labda kama akikumbwa na majeruhi.
Mshambuliaji wa kati, Gaudence Mwaikimba anaweza kuanza, huku nahodha John Bocco `Adebayor` akicheza namba kumi.
Winga wa kushoto anaweza kuanza Kipre Herman Tchetche anaweza kuanza tofauti na mechi za nyuma.
Kwanini Omog anaweza kuwatumia washambuliaji watatu kwa wakati mmoja?, sababu kubwa ni kutafuta mabao kwani ushindi pekee ndio matokeo ya maana kwake.
Watalazimika kushambulia kwa wakati wote ili kupata mabao ya mapema na kuibuka na pointi tatu muhimu.
Pia wapo wachezaji wengine wanaoweza kutokea benchi ambao ni Mwadini Ally,  Said Morad,  Jabir Aziz,  Brian Umony,  Kelvin Friday,  Mudathir Yahya, na  Khamis Mcha.
Kwa aina hii ya wachezaji wa Azam fc wanaotarajia kucheza leo, Ruvu Shooting watahitaji kutumia akili za ziada kuwazuia wasipate ushindi.

2 comments:

  1. azam washafungwa kabla mpira kuanza leo lazma azam afungwe akitaka asitake bado mtoto mdogo wakuibabaisha yanga africa tim bora tanzania

    ReplyDelete
  2. Azam ndiye mpya,mliharibu timu yenu kwa kuwasajili Okwi na Ngassa na faida yake ni kukosa ubingwa

    ReplyDelete