Search This Blog

Monday, April 7, 2014

NGORONGORO HEROES KUUMANA NA AFRIKA KUSINI IKIFANIKIWA KUITOA KENYA TAIFA

Nahodha na kipa namba moja wa Ngorongoro Heroes, Aishi Manula

 Na Boniface Wambura, Dar es salaam
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngongoro Heroes) imereja nchini leo mchana (Aprili 7 mwaka huu) kutoka Kenya mechi ya michuano ya Afrika dhidi ya wenyewe, na itaingia kambini Alhamisi.

Ngorongoro Heroes ambayo imewasili saa 8.25 kwa ndege ya Kenya Airways ilitoka suluhu na Kenya katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Kanyetta uliopo katika mji wa Machakos.

Kocha John Simkoko amesema benchi lake la ufundi linafanyika kazi upunguzi uliojitokeza ili wafanye vizuri kwenye mechi ya marudiano itakayochezwa Aprili 27 mwaka huu jijini Dar es Salaam. 
Iwapo Ngorongoro Heroes itaitoa Kenya, raundi inayofuata itacheza na Afrika Kusini. Fainali za Afrika kwa vijana chini ya miaka 20 zitafanyika mwakani nchini Senegal.

No comments:

Post a Comment