Search This Blog

Tuesday, April 8, 2014

MOURINHO ATAMBA KUPINDUA KIPIGO CHA 3-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI UEFA!!


Grumpy? Mourinho speaks ahead of the second leg against PSG on Tuesday
Ataweza? Mourinho akiongea na waandishi wa habari kabla ya mchezo wa leo usiku dhidi ya  PSG 
In or out? Eto'o (right) speaks to Fernando Torres and Ramires at Chelsea's Cobham training base
Ndani au nje? Eto'o (kulia) akizungumza na Fernando Torres pamoja na Ramires katika uwanja wa mazoezi wa Chelsea wa Cobham
Going through their paces: Jose Mourinho takes charge of Chelsea's training session on Monday
Jose Mourinho akiwa mazoezini na wachezaji wake jana

MTEGO!. Jose Mourinho amewata wachezaji wake kuwa na imani ya kuitupa nje Paris Saint-Germain katika mchezo wao wa marudiano wa robo fainali kesho usiku.

Mourinho amesisitiza kuwa kikosi chake kinaweza kupindua matokeo ya kufungwa mabao 3-1 katika mchezo wa kwanza, hivyo mashabiki wawe na imani kwa wachezaji wao katika kipute hicho kitakachopigwa uwanja wa Stamford Bridge 

  • Hata hivyo, safu ya ushambuliaji ya Chelsea imeongezewa nguvu baada ya Samuel Eto`o kufanya mazoezi kujiwinda dhidi ya PSG.

"Tunatakiwa kufurahia hali halisi. Sababu si muhimu sana. Kitu pekee ni kuwa na imani,  na naamini tunaweza. Wachezaji wangu wanaamini pia"

"Kama Paris watatolewa itawauma sana. Kama tutatolewa ndio kitu ambacho watu wengi wanatarajia"

"Nadhani baada ya mechi zote mbili tutakuwa na mabao mengi kuliko wao. Kama sina imani hiyo, sina sababu ya kwenda kwenye mechi na ninafuraha ya kwenda". Alisema Mourinho.
  • Naye Kocha wa PSG, Laurent Blanc  amesema hawaogopi kukabiliana na Chelsea  Stamford Bridge, hivyo mashabiki wao wajiandae kupokea matokeo mazuri.
  • Positive: Paris Saint-Germain manager Laurent Blanc insists his side won't sit back against Chelsea
    Ana matumaini: Kocha wa Paris Saint-Germain Laurent Blanc amesisitiza kuwa timu yake haitayumbishwa na Chelsea kesho
    Preparation: PSG's players get used to Stamford Bridge in a training session on Monday evening
    Maandalizi: Wachezaji wa PSG wakipasha katika dimba la  Stamford Bridge leo jioni

No comments:

Post a Comment