Search This Blog

Friday, April 11, 2014

KUIKOSA MICHUANO YA ULAYA MSIMU UJAO KUTAITHIRI MANCHESTER UNITED KIASI GANI?

Kwa takribani miaka 10 iliyopita ungeonekana mwendawazimu hata kwa kutamka tu kwamba Manchester United haitokuwemo kwenye timu nne kutoka England zitakazoenda kushiriki michuano ya klabu bingwa ya ulaya wakati klabu hiyo ikiwa chini ya Sir Alex Ferguson, lakini chini ya uongozi wa David Moyes kusema jambo hilo sio kitu cha ajabu na hata unaweza kuungwa mkono na 99% ya wapenzi wa soka kwa ujumla.

United mpaka sasa inashika nafasi ya 7 zikiwa zimebaki mechi 5 msimu kumalizika, na kila siku matumaini ya kuweza kumaliza ndani ya Top 4 yanazidi kufutika.
Baadhi ya watu wanadhani kufeli kwa United kufuzu kucheza ulaya kutawaharibia na kuwapeleka katika njia waliyopitia Liverpool kwa takribani miongo miwili iliyopita. Lakini kwa United inaweza kuwa tofauti.
Wakati mambo yalivyoanza kwenda mlama kwa Liverpool, walianza kuuza wachezaji wao bora - katika miaka ya hivi karibuni walimuuza Xabi Alonso, Javier Mascherano na Fernando Torres.  Manchester United kwa upande mwingine wamegoma kabisa kuuza wachezaji wao bora wameanza na Wayne Rooney kwa mkataba mrefy. Pia Liverpool hawakuwa misuli minene ya kifedha ukilinganisha na United ambayo ni klabu tajiri kupitiliza.

Liverpool walikuwa wakiuza assests zao kutokana matatizo ya kifedha. Rafa Benitez alifanya kazi nzuri kuliko sifa anayopewa, aliweza kutengeneza kikosi kizuri cha ushindani pamoja na kutokuwa na fungu kubwa la pesa kama ilivyokuwa kwa vilabu  Manchester United na Chelsea katika kipindi kile. Manchester United walionyesha jeuri yao ya fedha katika usajili wa rekodi wa £37 million wa Juan Mata na hawatoyumba kiuchumi kutokana na kukosa michuano ya ulaya kwa msimu mmoja. 

Mapato ya United katika mwaka wa fedha uliopita yalikuwa  £363.2 million. Fedha za mauzo ya haki ya matangazo ya TV ya michuano ya ulaya hazichangii hata robo ya mapato ya jumla, hivyo United ambao kila kukicha wanasaini mikataba mipya ya kibiashara wataendelea kutengeneza fedha nyingi kupitia uuzaji wa bidhaa zao kutokana na ufuasi mkubwa wa mashabiki walionao duniani, mauzo ya haki za matangazo ya mechi za ligi na michuano mengine ya ndani.

Usajili Juan Mata - mhispani huyu alijua wazi uwezekano mdogo wa United kumaliza kwenye Top 4 msimu huu.  Of course alihitaji kuondoka Chelsea kuelekea kombe la dunia, lakini ukweli kwamba alikuwa mchezaji wa daraja la juu aliyevutiwa na kujiunga na United pamoja na kutokuwepo kwa michuano ya ulaya kwenye klabu hiyo msimu ujao - hilo linaonyesha klabu bado ina uwezo wa kuvutia wachezaji wakubwa. United ni klabu kubwa yenye ufuasi mkubwa zaidi duniani na wachezaji wengi duniani bado watataka kujiunga na klabu hiyo.
Hata kama hilo halitoshi tuliona msimu uliopita kwamba kivutio kikubwa kwa wachezaji siku hizi ni fedha. Falcao alihamia Monaco, pamoja na kuwa anatakiwa na vilabu vingine vikubwa vilivyokuwa vinacheza ulaya. Falcao kiuwazi kabisa ameenda Monaco kufuata fedha pamoja faida ya kutokulipa kodi. Monaco hawana hata jina au sifa ya Manchester United, hivyo itakuwa rahisi kwa United kuvutia wachezaji kivyovyote, aidha kifedha au kisifa ya ukubwa wa klabu.

HITIMISHO
Kutokuwepo kwenye michuano ya Ulaya msimu ujao kwa hakika sio jambo zuri na kitu kikubwa kibaya kwa sifa ya United ambao kwa muda mrefu wamekuwa washiriki wa michuano ya ulaya. Tena kitu hiki kimetokea wakati m'baya kipindi ambacho timu inajengwa upya. Lakini kitu ambacho nina uhakika nacho - kwa misuli mikubwa ya fedha waliyonayo na ukubwa wa timu basi haitowachukua muda mrefu kurudi kwenye zama zao za ushindi. 

2 comments: