Search This Blog

Wednesday, April 2, 2014

FC BARCELONA YAFUNGIWA VIPINDI VIWILI VYA USAJILI NA FIFA - NAMNA WATAKAVYOATHIRIKA


Klabu ya FC Barcelona imefungiwa na FIFA kufanya usajili wa mchezaji kwa vipindi vijavyo viwili vya usajili kuanzia dirisha kubwa la usajili lijalo mpaka January 2015 kwa kuvunja sheria ya uhamisho na usajili wa wachezaji chini ya miaka 18.

Kifungo hicho kinafuatia uchunguzi uliofanywa na Fifa Transfer Matching System (Fifa TMS).


Kutokana na Adhabu hii, Barcelona hawaruhusiwi Kuuza au Kununua Mchezaji yeyote yule hadi Vipindi viwili vya Uhamisho vimalizike na hii inamaanisha Adhabu yao itaisha Juni 2015.

Pamoja na kufungiwa huko, Barca pia imetozwa faini ya Paundi 305,000.

Pamoja na Barca, pia Shirikisho la Soka la Spain, RFEF, nayo imeadhibiwa kwa Kosa hilo hilo la Barca.

RFEF imepigwa Faini Paundi 340,000 na kuamriwa kuweka sawa mfumo wao Uhamisho unaohusu Wachezaji Vijana ndani ya Kipindi cha Mwaka mmoja.

9 comments:

  1. acha kukopi na kupest bro(kichwa cha habiri cha kiswahili lkn vilivyo Baku vyote imetumika lugha ya kigen)KWANI HII BLOG NI YA KIGENI AU

    ReplyDelete
  2. umeshindwa hata kutafsiri hayo maneno kwa kiswahili? sasa umetuwekea ya nini?? kweli umevamia fani ya watu.... hustahili kuwa mchambuzi wa soka " copy and paste" hili inaonyesha kwamba hujui lugha ya kiingereza.. pole sana

    ReplyDelete
  3. Achen ujnga mnataka awafanyie con versions za hzo pound au? Kwan ww ukitaka kutaja abbriviation ya shrka la afya dunian utasema SLAD au WHO, Pigen kmya bg up shaffih

    ReplyDelete
  4. Kwani tatizo liko wapi?
    Kuna mtu ambae hajaelewa? Au mlitaka aandike kwa zenu za makabila ndo mumuelewe,
    Ebu acheni ujinga wa kukosoa wenzenu,kama nyie mnajua zaidi anzisheni blog zenu.

    ReplyDelete
  5. Wadau mlopita inaonyesha mna uwezo mdogo haya.wa.kusoma.kiswahili,kila.kitu.kimeandikwa vizur hata kwa vilaza wanaweza.elewa, big up Dauda

    ReplyDelete
  6. Msiwe wa kulaumu kila kitu tumia mud a mwingi kujifunza kuliko kukosoa. Jiulize hizo habari ulifahamu kabla.

    ReplyDelete
  7. Mnajifanya wataalam wa kiswahil kumbe hakuna lolote.

    ReplyDelete
  8. Ifike mahali tuwe seriouz kwani hapo kisichoeleweka nin maana waswahili wanasema asiye juwa maaana haambiwi maana so.. mi sjaona tatizo hapo kwani hata choon unaweza sema kwa mkato maliwato... ilaa kwa wale pumbaaa less wanaweza tamka big up sanaaa Daudaaaaaa

    ReplyDelete