Search This Blog

Thursday, April 3, 2014

DAUDA TV: NINI MAONI YAKO JUU YA HILI BAO ALILOFUNGWA JUMA KASEJA KWENYE MCHEZO DHIDI YA JKT MGAMBO.

8 comments:

  1. Tatizo hapo ni seriousness kwenye game hakuna huyo mfungaji kaonyesha seriousness yake ambayo imekutana na laziness hivyo kuonyesha nini? Mchezaji unapaswa kufanya muda wote wa mchezo vinginevyo itabidi kaseja akubali AMECHUJA level yake sasa ni kudakia timu zenye hadhi ya chini kama alivyofanya Peter Shmerchiel toka Msn united

    ReplyDelete
  2. huyu jamaa amekula hela simple.. hili ni moja kati ya magoli ya kizembe kabisa niliyo yaona in my life time so far

    ReplyDelete
  3. Goli la Kaseja hilo wala hakuna mjadala. Yondani anaonewa tu. Mara ya ngapi Kaseja amefungwa magoli ya namna hiyo? Ina maana na ukongwe wote huo anashindwa kujirekebisha? Mnakumbuka mtani jembe? Mrungura tu huo. Mi sina imani kabisa na huyu bw. Mtanisamehe tu kwa kweli mi pindi nimwonapo langoni matumaini ya ushindi unitoka kabisa.

    ReplyDelete
  4. Siafiki kwamba Kaseja kala hela, kwani alitegemea kurudishiwa mpira? sema uzembe na kukosa umakini. Japokuwa ni bahati mbaya lakini dah inavunja nguvu wengine. Bahati yake haikuwa Simba na Yanga maana washabki na viongozi wala wasingeangalia hizo ishu. Poleni sana Yanga ndio ukubwa hata Arsenal alifungwa bao 6 na chelsea kizembe zembe tu.

    ReplyDelete
  5. Duh hiyo kweli kazi. Usajili mwingine kweli ni matumizi ya pesa yasiyokuwa makini. Simba walikuwa na kila sababu ya kumtema!

    ReplyDelete
  6. huyu kaseja ni mamluki hii inajidhihirisha kabisa mpira mwepesi kama huu unashindwa kuucheza kwa umakini. alikuwa anauwezo wa kuupeleka upande wa pili wa uwanja alipokuwa canavaro au katikati kwa domayo yeye bila kufikiria anampatia mfungaji mpira hii ni aibu kwa mchezaji mkubwa kama kaseja. After all, huyu sio kaseja ninayemjua kachuja sana hana hadhi ya kucheza yanga ni bora aonyeshwe njia mapema akacheze ndanda fc au stand united.

    ReplyDelete
  7. Hata Mustafa Barthez asingefungwa goli la aina hii au lile la Nani Mtani jembe.Kaseja anawakatisha tamaa wenzake.Inaonekana kocha wa Mgambo alishawaelekeza kitu strikers wake kuhusu udhaifu huu wa Kaseja na mabeki wake ndio maana walikuwa wanavizia kama wanajua nini kitatokea.Makosa ya aina hii yamekuwa yanajirudia sana kwenye defence ya Yanga,mara nyingi wanapenda kurudisha mipira nyuma na wakati mwingine wanaipitisha katikati ya penalty box huku kipa akiwa ametoka golini.Canavaro na Joshua sasa hivi wamejirekebisha lakini Yondani na Twite bado.Uchezaji wa kuanzisha mashambulizi kutokea golini kwenu unafaa unapokuwa na mabeki wazoefu lakini wenye umri mdogo na wenye control nzuri ya mpira na uwezo wa kuchezea mpira.Umri wa mabeki wengi wa Yanga uko juu na Yondani na Twite hawana kasi ya kutosha timu inapopoteza mpiraUkiangalia hapo juu unaona kabisa Canavaro yuko mbali huku Twite akiwa anaangalia mashabiki.Yondani huwa ana tatizo la kujiamini kupita kiasi na wakati mwingine huwa analazimisha kupiga chenga na anaponyang'anywa mpira hana mbio za kurudi kukaba na wakati huo wenzake wanakuwa wameshapanda

    ReplyDelete
  8. kaseja hapa wewe unasemaje kuhusu haya maoni yako ?wewe amua kama unekuya kweye sahani unayokulia au inakojolea msaala unaosalia au la hasha sasa hebu tupe jibu.

    ReplyDelete