Search This Blog

Monday, April 7, 2014

ANELKA AMFUATA RONALDINHO BRAZIL - AJIUNGA NA ATLETICO MINEIRO

Klabu ya Atletico Mineiro ya Brazil imethibitisha usajili wa mshambuliaji wa kifaransa Nicolas Anelka kwa uhamisho wa bure.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 35 amekuwa hana klabu kwa muda sasa tangu alipofukuzwa na klabu ya West Bromwich Albion mwezi uliopita, muda mfupi baada ya kutangaza kupitia mitandao ya kijamii kwamba anasitisha mkataba wake na klabu hiyo ya EPL.

Kwa mujibu wa Raisi wa Atletico Mineiro Alexandre Kalil, mshambuliaji huyo amekubali kujiunga na mabingwa wa Copa Libertadores, ambao pia wana mchezaji bora wa zamani wa duniani  Ronaldinho.


Hii itakuwa mara ya pili kwa Anelka na Ronadinho kucheza pamoja - mara ya kwanza ilikuwa katika klabu ya PSG ya Ufaransa.

No comments:

Post a Comment