Search This Blog

Wednesday, March 12, 2014

YANGA KUWASILI TANZANIA KESHO ALFAJIRI KUTOKEA CAIRO


Kikosi cha wa waliokuwa wawakilishi pekee wa mashindano ya kimataifa nchini Tanzania Young Africans kinatarajiwa kuwasili kesho alfajiri jijini Dar es salaam kwa shirika la ndege la Egypt Air kikitokea jijini Cairo nchini Misri kilipokuwa na mchezo wa marudiano dhidi ya Al Ahly na kutolewa kwa mikwaju ya penati 4-3 mchezo uliofanyika katika Uwanja wa El Max jijini Alexandria.

Mara baada mchezo huo uliofanyika siku ya jumapili na wenyeji kufuzu hatua ya 16 kwa mikwaju ya penati, msafara wa viongozi wa Young Africans pamoja na wachezaji waliwasili jana mchana jijini Cairo na kufikia katika hoteli ya Marriot iliyopo eneo la Zamalek.

Balozi wa Tanzania nchini Misri Bw Mohamed Hamza aliandaa chakula cha jioni kilichojuimsha wachezaji, viongozi, maofisa ubalozi na familia zao, waandishi wa habari pamoja na baadhi ya watanzania waishio nchini Misri.

Akiongea kwa niaba ya serikali Balozi Hamza aliwaambia wachezaji wasivunjike moyo kwani wamepambana kadri ya uwezo wao, timu ilicheza vizuri lakini mwisho wa siku bahati haikuwa yao hivyo wajipange upya ili mwakani waweze kufanya vizuri zaidi ya mwaka huu.

Leo asubuhi kikosi cha Young Africans kilifanya mazoezi katika uwanja wa Al Ahly uliopo makao makuu ya klabu hiyo eneo la Zamalek kisha mara baada ya mazoezi viongozi walipata fursa kuongea na viongozi wa Al Ahly wakiwemo makocha ambao walitoa pongezi kwa wachezaji wa Yanga kwa kiwango walichokionyesha katika michezo yote miwili.

Uongozi wa Yanga unawashukuru wapenzi, wanachama, washabiki na wadau wote wa soka waliokuwa pamoja katika kuiombea timu ya Yanga kufanya vizuri katika mchezo ambao vijana walitolewa kwa mikwaju ya penati, wasivunjike moyo nguvu zote zinaelekezwa kwenye Ligi Kuu ya Vodacom siku ya jumamosi dhidi Mtibwa Suga ya Morogoro lengo la uongozi na wachezaji ni kutwaa Ubingwa wa VPL kwa msimu wa pili mfululizo.

2 comments:

 1. dauda,

  nadhani wewe ulikuwa uwanjani na uliweza ushuhudia baadhi ya matukio yaliyojiri kwenye mechi ya al ahly na yanga.
  Unalizungumzia vipi suala hili ambalo zimezua mjadala mzito Tanzania na barani Africa kwa ujumla juu ya shutuma za imani za kishirikina michezoni?

  Hivi juzi tumeona golikipa wa raja cassablanca na golikipa wa yanga wakifanya vitendo ambavyo vinaashiria imani za kishirikina,je sharia za CAF zinasemaje juu ya vilabu ama mchezaji anapoonekana wazi wazi kufanya vitendo hivyo???

  tazama video hii inavyoonyesha vitendo hivyo.
  http://www.supersport.com/football/caf-champions-league/news/140311/Black_magic_and_the_Caf_CL

  regards,

  Godfriend A

  ReplyDelete