Search This Blog

Saturday, March 8, 2014

TUTAWASHAMBULIA AHLY KUANZIA DAKIKA YA KWANZA ILI TUPATE BAO LA MAPEMA.Kocha wa Yanga,Hans Van Pluijm amesema hatabadili mfumo uliotumika Dar Es Salaam kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Al Ahly,
‘’Kwenye mchezo wa Dar Ahly waliwatumia  wachezaji tisa nyuma ya mpira na bado tulifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi,naamini kwenye mchezo wa marudiano watalazimika kutushambulia nasisi tutatumia mwanya huo huo kuwashambulia.

Napendelea mchezo wa kushambulia,kama unataka kushinda mechi ni lazima ufunge magoli,lakini pia timu yetu ni nzuri sana kwenye idara ya ushambuliaji kuliko idara ya ulinzi,ningependelea mchezo wa kushambulia lakini wachezaji wanahitaji kuwa na nidhamu kubwa ya kufuata maelekezo’’.

Van Pluijm pia amesema kikosi chake kipo vizuri na hakiogopi majina makubwa ya wachezaji wa Ahly, ‘’Majina hayachezi mpira bali timu ndio inacheza, kinachotakiwa ni wachezaji kujiamini na kuamini wanaweza,wakifanikiwa katika hilo naamini tutawashangaza ‘’.2 comments:

  1. Shaffih tunaomba live coverage baadae jioni.Kila la kheri

    ReplyDelete
  2. Mungu ibariki dar yng africa,

    ReplyDelete