Search This Blog

Tuesday, March 4, 2014

TFF KUWACHUKULIA HATUA ZAIDI WAWILI TWIGA STARS

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linatafakari hatua zaidi za kinidhamu dhidi ya wachezaji wawili wa kikosi cha Twiga Stars walioondolewa kwenye timu hiyo na Kocha Rogasian Kaijage.

Kocha Kaijage aliwatimua kambini wachezaji Mwapewa Mtumwa na Flora Kayanda kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu wakati Twiga Stars ikijiandaa kwa mechi ya marudiano ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC) dhidi ya Zambia.

Twiga Stars ilipoteza mechi ya kwanza ugenini mabao 2-1 na kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya marudiano iliyochezwa Februari 28 mwaka huu Uwanja wa Azam Complex, hivyo kutolewa katika mashindano hayo kwa jumla ya mabao 3-2.

TFF tunaunga mkono hatua iliyochukuliwa na Kocha Kaijage dhidi ya wachezaji hao wakongwe wa Twiga Stars, kwani katika shughuli yoyote ile inayohitaji ufanisi nidhamu ni kitu cha kwanza.

Twiga Stars itacheza mechi za mchujo za michezo ya 11 ya Afrika (All Africa Games) ambayo itafanyika mwakani nchini Congo Brazzaville.

3 comments:

  1. NA NYIE TFF MTACHUKULIWA HATUA NA NANI?

    ReplyDelete
  2. Wanaopaswa kuadhibiwa ni viongozi wa TFF,hasa Rais,Kamati ya Ufundi na Kamati ya Mashindano kwa kuitelekeza timu hii. Adhabu waliyopewa wachezaji hawa kwa kuondolewa kambini na kwenye safari inatosha,suala hili lisitumike kuficha udhaifu wa TFF wa kushindwa kuwajibika ipasavyo kuandaa timu hii na hatimaye imetolewa kwenye mashindano.Malinzi anapiga kelele za mikakati kibao ya kuipeleka Tanzania Afcon 2015 wakati hii midogo tu ya wanawake imemshinda.Awajibike

    ReplyDelete
  3. Kipaumbele ni timu za vijana, sio vi bibi kizee.

    ReplyDelete