Search This Blog

Monday, March 3, 2014

SAINI 6,000 ZA MASHABIKI ZAKUSANYWA KATIKA OMBI LA KUMZUIA CLEVERLEY KUITWA KATIKA KIKOSI CHA ENGLAND CHA KOMBE LA DUNIA

Maelfu ya saini za mashabiki wa soka zimekusanywa katika ombi rasmi la kutaka kiungo wa Manchester United  Tom Cleverley kufungiwa kucheza katika michuano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Brazil mwaka huu.

Mpaka sasa ombi hilo limeshakusanya jumla ya saini 6,000 ndani ya kipindi cha masaa 36, lilikusanya saini 4,000 ndani ya masaa 24, na lilosomeka kama ifuatavyo: 'Tom Cleverley, ambaye tayari ameshaichezea England mechi 13, amekuwa akiteuliwa na Roy Hodgson katika vikosi vya England bila kuwa na sifa yoyote ya maana. 

'Tunaamini katika taswira nzuri ya kikosi cha taifa hili kubwa na kwamba tunataka azuiwe kushiriki katika michuano ijayo ya kombe la dunia. 
'England inaaminika kuwa ni timu mbovu katika michuano mikubwa, hivyo aibu zaidi inaweza kuepukika kwa kutomjumuisha yeye na kiwango dhaifu kitachoshusha jitihada za timu nzima.' 

Kama ilivyo kwa wachezaji wenzie wengi, Cleverley ameshindwa kurudia kiwango chake kizuri alichokuwa nacho miaka miwili iliyopita, kilichomfanya Sir Alex Ferguson kumuita 'special player'

Cleverley amefunga goli moja tu katika michezo 32 aliyoichezea klabu yake na amekuwa akisemwa mpaka na mashabiki wa timu yake, hasa kwenye mtandao wa Twitter.

Pamoja na kusemwa sana, kiungo huyo mwenye miaka 24 amechaguliwa na kocha Hodgson alhamisi iliyopita kuunda kikosi cha Denmark wiki hii, na inaonekana ana nafasi ya kwenda Brazil.  

No comments:

Post a Comment