Search This Blog

Monday, March 17, 2014

MOYES AENDELEA KUVUNJA REKODI ZA UNITED - MAN UNITED KWENYE NAMBA


1.   Mchezo wa kwanza kwa Manchester United kupoteza nyumbani dhidi ya Liverpool baada ya kushinda michezo sita  ndani ya miaka miaka mitano.
– Michezo mitatu mfululizo ya Manchester united wanayocheza nyumbani dhidi Liverpool, Olympiakos na Manchester City ndani ya siku kumi.
5- Mchezo wa tano Manchester United wamefungwa nyumbani kwenye ligi msimu huu.
7. Nafasi ambayo Manchester united wameikalia kwa muda mrefu kwenye msimamo wa ligi kuu ya England.
9. Idadi ya michezo ya ligi kuu ambayo Manchester United wamepoteza msimu huu.
13. Ni idadi ya michezo ambayo Manchester United wamepoteza kwenye michuano yote kwenye msimu wa 2013/2014.
14 – ni alama ambazo Manchester United wameacha na  Liverpool baada ya mchezo wa jana.
20 – idadi ya mataji ya ubingwa wa ligi kuu waliyoyatwaa Manchester United, mawili zaidi ya waliotwaa Liverpool
23 – ni miaka 23  tangu Manchester United washindwe kumaliza kwenye nafasi ya tatu.
Paundi milioni 42 - ambazo Man Utd walizipata kupitia haki za television, pamoja mapato waliopata kwenye ligi ya mabingwa barani ulaya.

No comments:

Post a Comment