Search This Blog

Thursday, March 20, 2014

MAN UNITED VS WEST HAM: SAM ALLARDYCE ANAKUTANA NA MWANAFUNZI WAKE MOYES ALIYEMTOA SCOTLAND NA KUMLETA ENGLAND


Zikiwa zimebakia siku kadhaa kabla ya mechi ya West Ham United vs Manchester United wikiendi hii, kocha wa West Ham  Sam Allardyce, ametoa historia ya kuvutia kuhusu yeye na David Moyes.
Allardyce anasema mwaka 1993, wakati akiwa kocha wa timu ya vijana ya Preston, alienda kumuangalia Moyes akiichezea Dunfermline dhidi ya Falkirk ili aone uwezo wake kama anafaa kusajiliwa, na alitumwa na kocha mkuu wa timu ya Preston John Beck.

Na pamoja Moyes kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kushika mpira makusudi katika kipindi cha kwanza dakika ya 38, Allardyce aliridhishwa na uwezo wake na akampelekea ripoti nzuri kocha mkuu Beck.
Moyes alipokuwa akiichezea Preston ambayo Allardyce alikuwa kocha msaidizi
Moyes hatimaye alihamia Preston, na baada ya mechi 159 mscotish huyo akawa kocha wa timu hiyo, lakini alikosa nafasi ya kupanda ligi kuu ya England baada ya kufungwa kwenye play-offs na Everton mnamo 2002.
Kuelekea mchezo ambao utawakutanisha Allardyce na Moyes wakati United itakapoifuata West Ham Upton Park, kocha wa West Ham anakumbuka alivyomuona Moyes mara ya kwanza. 
Allardyce alisema: 'Alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya dakika ya 38 za mchezo. Niliendesha gari mpaka Scotland,  John Beck alinituma nikamtazame. 
'Lakini ndani ya hizo dakika 38 nilijua kwamba angefaa kuitumikia Preston." 

1 comment:

  1. SHAFFIH U NDO UTABIRI WANGU LEO UEFA.(1)Man utd & PSG.(2)CHELSEA&BARCELONA.(3)BAYERN&DORTMOND.(4)REAL MADRID&ATRETICO MADRID.

    ReplyDelete