Search This Blog

Tuesday, March 25, 2014

KORTI YAAGIZA TFF IKAMATE MIL 106/- KULIPA WACHEZAJI YANGA


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tumepokea amri ya Mahakama Kuu (Kitengo cha Kazi) kukamata sh. milioni 106 za klabu ya Yanga kutokana na mapato ya mlangoni kwenye mechi zake ili kuwalipa waliokuwa wachezaji wake Stephen Malashi na Wisdom Ndlovu.

Tayari tumeanza utekelezaji wa amri hiyo ambapo katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) dhidi ya Rhino Rangers iliyochezwa Machi 22 mwaka huu mjini Tabora tumezuia sh. 9,221,250 ambazo ndizo zilizokuwa mgawo wa Yanga katika mchezo huo ulioingiza jumla ya sh. 38,655,000.

Wachezaji hao walifungua kesi kortini kupinga mikataba yao na klabu hiyo kuvunjwa bila kulipwa haki zao za kimkataba. Malashi na Ndlovu walishinda kesi hiyo, hivyo korti kuwapa tuzo hiyo ya sh. milioni 106.

Tunawakumbusha wanachama wetu (klabu za Ligi Kuu, vyama vya mpira wa miguu vya mikoa na vyama shiriki) kuzingatia mikataba wanayoingia na watendaji wao wakiwemo wachezaji, makocha na maofisa wengine.


Iwapo wanataka kuvunja mikataba ya ajira wafuate taratibu kwa vile hakuna mkataba ambao hauelezi jinsi ya kuvunjwa iwapo upande mmoja unataka kufanya hivyo

3 comments:

  1. NI KWELI YANGA WANADAIWA JE KISHERIA TFF WANAKIBALI CHA KUWA COURT BROKERS.....? WALITAKIWA WADAI WAPEWE KIBALI WAWAPE KAZI BROKERS WALIOKISHERIA......EG MAJEMBE AUCTION....SIDHANIU WANASHERIA WATUPE MUONGOZO HAPA KAMA KWELI MAHAKAMI INAWEZA KUWADIRECT TFF KUFANYA HIVYO AU TFF WALIENDA KUOMBA KIBALI KUWA COURT BROKERS...?

    ReplyDelete
  2. Wajifunze sasa kuacha uhuni!

    ReplyDelete
  3. Ni kweli TFF sio court broker ila ukitaka njia hiyo deni litakuwa kubwa zaidi maana kuna gharama za court broker ambazo itabidi pia zibebwe na Yanga.

    ReplyDelete