Search This Blog

Monday, March 24, 2014

KAMBI YA MAREKEBISHO YA TAIFA STARS YAANZA TUKUYU

Na Mwandishi maalumu, Tukuyu

Wachezani 29 kati ya 34 waliochaguliwa katika programu maalumu ya marekebisho ya timu ya Taifa inayoendeshwa na TFF wameshaanza mazoezi makali katika Wilaya ya Rungwe, Mbeya.


Wachezaji hao, ambao wametokea katika mikoa mabali mbali, waliingia kambini siku ya Jumamosi huku wakiongozwa na Mwalimu Salum Mayanga akisaidiwa na Patrick Mwagata, ambaye ni kocha wa makipa, Meja Joakim Mashanga ambaye ni daktari wa team na Fred Chimela ambaye ni Meneja Vifaa.


Timu ya Taifa, Taifa stars, inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro Premium Lager kwa mwaka wa pili mfululizo sasa, inatarajiwa kupata mabadiliko makubwa sana ndani ya miezi miwili ijayo ili ipatikane timu bora itakayoshiriki katika mechi za kufuzu kupata tiketi ya kucheza Kombe la Afrika.


Makocha wazoefu walikusanyika Lushoto takriban wiki mbili zilizopita na kufanya zoezi la kuwachagua vijana 34 ambao baadaye watachujwa na kubali 20.


Watakaochaguliwa watajiunga na Taifa Stars ya siku zote na kutengeneza timu ya wachezaji 45 ambao watahujwa tena ili ipatikane Timu ya Taifa yenye wchezaji 25.


Zoezi hili linatarajiwa pamoja na mambo mengine kuimarisha uzalendo miongoni mwa wachezaji watakaochaguliwa na hili linafanyika kwa kuhakikisha wachezaji wote wanaimba wimbo wa Taifa kila asubuhi na jioni kabla ya kuanza mazoezi.


Kila chumba cha wachezaji pia kina bendera ya Taifa, taratibu za kambi na wimbo wa Tanzania Tanzania ambavyo vinasaidia kuimarisha uzalendo miongoni mwa wachezaji.

Kocha Mayanga alisema kuwa vijana wote wako salama na wanategemea kuwapata wachezaji wazuri baada ya kambi hii.


“Tunapongeza wadhamini wetu Kilimanajro Premium Lager ambao wamefanikisha zoezi hili kwani tuna imani tutapata vipaji vikubwa mno baada ya zoezi hili na timu yetu ya taifa itakuwa bora zaidi,” alisema.


Wachezaji wamepiga kambi katika hoteli ya Landmark, mjini Tukuyu na wanafanya mazoezi katika Chuo Cha Ualimu Tukuyu.


Zoezi hili limeleta msisimko mkubwa mjini Tukuyu huku mashabiki wa mpira wakisema wana imani sasa itapatkana timu bora zaidi kwa sababu ya utaratibu uliotumika.

2 comments:

  1. Mmmmh!!ni ngumu kidogo lakini,nahofu tutaishia njiani then tukaendelea na mazoea yetu

    ReplyDelete