Search This Blog

Monday, March 3, 2014

KAKA YAKE TONI KROOS AMZUNGUMZIA NDUGUYE KUHAMIA MANCHESTER UNITED

Kaka wa mwanasoka Toni Kroos, Felix Kroos  amesema kwamba ndugu yake, ambaye ni kiungo wa Bayern Munich, anaweza kujiunga na Manchester United katika dirisha lijalo la usajili.

Kiungo huyo mjerumani, ambaye alifunga bao zuri katika mchezo wa raundi ya 16 ya ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya Arsenal, amekuwa akihusishwa na uhamisho wa kujiunga na klabu ya Old Trafford, huku mazungumzo ya mkataba mpya baina yake na Bayern Munich yakiwa hayaendi vizuri, mkataba wake wa sasa unaisha 2015.

Huku mazungumzo ya mkataba mpya yakiwa yamegoma Allianz Arena, kaka yake, ambaye anaichezea Werder Bremen, sasa amefunguka na kusema amekuwa na mazungumzo na mdogo wake kuhusu kuhamia katika ligi kuu ya England.

Felix aliiambia Sky Germany: "Tumeshaongea kuhusu hilo jambo la Toni kuhamia Manchester United].

"Manchester imekuwa timu ya ndoto yangu tangu nilipokuwa mtoto. Japokuwa mie sijampa ushauri wowote.

"Atachukua maamuzi mazuri kwa ajili yake." 

No comments:

Post a Comment