Search This Blog

Sunday, March 2, 2014

ERICK KYARUZI AIPATIA USHINDI KAGERA LEO KAITABA, KOCHA FREDY FELIX MINZIRO AUTAZAMIA KWA MASHABIKI MTANANGE HUU!!

Picha ya Pamoja na Waamuzi na Timu Kapteini.
Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi kuu soka Vodacom Tanzania Bara imeendelea leo, Katika Uwanja wa Kaitaba Timu ya Kagera Sugar imeendelea kuutumia uwanja wao vyema wa Kagera Sugar Baada ya kuwafunga Maafande JKT Ruvu bao 1-0, Bao lililofungwa na Mtoto wa Nyumbani hapa Kagera aliyetokea timu ya Toto ya jijini Mwanza msimu uliopita. 
Kona iliyopigwa na Mohamed Hussein (Shabalala) na  Daudi Jumanne kuupoza kwa kichwa kwa kumgawia Erick Kyaruzi na hatimae kuutokomeza mpira huo langoni mwa Lango la Maafande JKT Ruvu katika dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza katika dakika ya 43.
Mpaka dakika za mapumziko zinamalizika timu ya Kagera Sugar Ndio ilienda mapumziko ikiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu.
Kipindi cha pili JKT Ruvu walilazimika kumtoa Kipa wao na kumwingiza kipa mwingine baada ya kuumia kwa kipa wao kwa nza katika kipindi cha kwanza.
Kipindi hicho hicho cha kwanza mwanzoni akikuwa chema baada Kocha wao JKT Ruvu Fredy Felix Minziro  kutolewa nje ya Uwanja na kuutazamia mpira huo kwa mashabiki baada ya kufanya kile ambacho kilikuwa si sawa kwa mwamuzi Kamisaa wa mchezo huo.
Kikosi kilichoanza cha Maafande JKT Ruvu
Benchi la Kagera Sugar
Mtanange ukiendelea....
Mchezaji wa JKT Ruvu Amos Mgisa akiwaendesha wachezaji wa Kagera Sugar
katika kuutafuta mpira hapa...kila mchezaji anautaka...
Mchezo ukiendelea....
Kipa wa JKT Ruvu Shabani akipatiwa huduma baada ya kuumia bega
Mganga wa Timu ya JKT Ruvu akimpa huduma ya haraka Kipa
Kipa wa JKT Ruvu akijisikilizia maumivu..
Mapande ya Kagera Sugar yalimpa taabu kipa wa JKT Ruvu
Kona iliyozaa bao kwa Kagera Sugar iliyopigwa na Shabalala wa Kagera Sugar
Erick Kyaruzi akishangilia baada ya kufunga bao
Kapteni wa Kagera Sugar akimpgeza Erick Kyaruzi baada ya kuwapachikia bao la kichwa
Asante Baba!!!
Erick Kyaruzi
Erick Kyaruzi akirudi uwanjani baada ya kuwapa bao Kagera Sugar
Nyimbo zikiendelea..................ole ole oleeee....
Yes yes yes yes !!!!!!!
Mashabiki wa Kagera Sugar wakishangilia baada ya bao lililofungwa na Erick Kyaruzi
Mashabiki wa Kagera Sugar wakiendelea na nyimbo zao kuitaka Kagera ishinde tena leo
kipindi cha pili mapema kipa alieumia bega aliotolewa na kuingia kipa mwingine wa JKT Ruvu
Patashika kwenye lango la JKT Ruvu  kipa akipangua..
KOCHA FREDY FELIX MINZIRO  akiendelea kutazama kipindi cha pili jukwaani kwa mashabiki
KOCHA FREDY FELIX MINZIRO
Kipa wa pili wa JKT Ruvu nae alikuwa na kazi langoni mwake!!
Kiongozi wa JKT Ruvu aliyechukua nafasi ya Felix Minziro
Aliechukua nafasi ya KOCHA FREDY FELIX MINZIRO
Hapa Hupiti!
Karage Mgunda wa JKT Ruvu akiondosha mpira hapa kwenye eneo la kona
Pisha mbali...!
Majanga!
Adam Kingwande mchezaji wa Kagera Sugar akimkaba George Minja wa JKT Ruvu
Mchezaji wa JKT Ruvu akimzuia George Kavilla
Mtanange umemalizika...

No comments:

Post a Comment