Search This Blog

Thursday, February 6, 2014

SOKA KWENYE NAMBA: WESLEY SNEIJDER AFUNGA HAT TRICK YA PILI TANGU AANZE KUCHEZA SOKA LA KULIPWA



25
 Rekodi ya ushindi mfululizo wakiongoza ligi, iliyowekwa na FC Barcelona ilifikia tamati baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Valencia na kuporwa uongozi wa Ligi na Atletico Madrid. Ushindi wa Valencia ulikatiza rekodi ya kushinda mara 25 mfululizo kwenye la liga zilizochezwa kwenye dimba la Nou Camp. Valencia imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda nyumbani kwa Barca tangu Real Madrid walipofanya hivyo mnamo April 2012. Siku iliyofuatia Atletico Madrid wakashinda 4-0 dhidi ya Real Sociedad, wakaenda kushika usukani mwa ligi kwa mara ya kwanza tangu waliposhinda makombe mawili msimu wa 1995/96.
3
 Mabao matatu yaliyofungwa na Wesley Sneijder katika ushindi wa Galatasaray wa 6-0 dhidi ya Bursaspor jumapili iliyopita - ilikuwa ndio hat trick ya pili ya Sneijder tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa. Pia ilikuwa hat trick ya kwanza katika kipindi cha miaka saba, mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa kwenye mchezo wa ushindi wa 4-1 wa Ajax dhidi ya Feyenoord mnamo 4 February 2007. Ushindi huo wa Gala ulikuwa mkubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni, mara ya mwisho walishinda ushindi mkubwa ilikuwa walipoifunga Manisaspor 6-3 February 2008.
3
 Miaka mitatu, miezi mitatu ya mechi 61 za matokeo chanya - huo ndio muda kamili tangu mara ya mwisho Manchester City waliposhindwa kufunga goli katika mchezo wa ligi kuu ya England uliochezwa nyumbani kwao, lakini kikosi cha Jose Mourinho kikavunja rekodi hiyo usiku wa Jumatatu, Lakini pia kikosi cha Jose Mourinho hakikuvunja rekodi hiyo tu bali pia walivunja rekodi ya City ya kushinda kwenye mechi ya ligi ya nane mfululizo pia kipigo cha pili katika mechi 22 walizocheza Etihad. 

No comments:

Post a Comment