Search This Blog

Wednesday, February 19, 2014

RIVALDO AWEKA REKODI YA KUCHEZA TIMU MOJA NA MWANAEGwiji la soka nchini Brazil Rivaldo ametengeneza historia baada ya kucheza timu moja na mtoto wake kwenye dimba lililopewa jina la baba yake mzazi.


Rivaldo mwenye umri wa miaka 41, aliingia kuchukua nafasi ya Mogi Mirim kwenye mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa ligi ya jimbo la Sao Paolo,mchezo huo ulichezwa kwenye dimba la Romildo Ferreira.  


Ilikuwa ni mara ya kwanza Rivaldo kucheza mchezo wa ligi kwenye timu moja na mwanae Rivaldo Junior mwenye umri wa miaka 18.


Mnamo mwaka 1996, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Barcelona Eidur Gudjohnsen aliingia uwanjani kuchukua nafasi ya baba yake Arnor  kwenye mchezo wa timu ya taifa ya Iceland dhidi ya  Estonia,kwahiyo ndoto yao ya kucheza pamoja haikufanikiwa.

No comments:

Post a Comment