Search This Blog

Monday, February 10, 2014

MORO VETERAN WAICHAPA GOLANI VETERAN YA KIMARA BAO 4


Kikosi cha Timu ya Golani Veteran ya Kimara Jijini Dar es salaam Kilichofanya Ziara Mkoa wa Morogoro.
Kikosi cha Timu ya Moro Veteran Kilichoanza . 
Moja ya Hekaheka katika Lango la Golani Veterani katika Mchezo wa Kirafiki Uliopigwa Katika Uwanja Wa Jamuhuri Mkoani Morogoro.
Beki wa Golani Veteran Akiondosha Moja ya Hatari Katia Lango lake.
Mshambuliaji  wa Zamani wa Timu ya Polisi Morogoro Ambaye kwa sasa anaichezea Timu ya Moro Veteran Mokil Rambo Akitafuta Mbinu za Kuwatoka Mabeki wa Golani Veteran Katika Mchezowa Kirafiki  Uliochezwa Katika Uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro .
Mchezaji wa Zamani wa Timu za Morogoro Adam Seleman wa Moro Veteran akiwa katika Hekaheka  za Kutafuta Mbinu za Kuwatoka Mabeki wa Timu ya Golani Veterani ya Kimara Dar es Salaam katika Mchezo wa KirafikiUliopigwa Katika Dimba la Jamuhuri Mkoani Morogoro.

Wachezaji wakongwe wa Golani Veteran Ambao walikuwa Kivutio Katika Mchezo wa leo

Mwenyekiti wa Timu ya Moro Veteran Khamis Madole akipongezwa na Mchezaji Mwenzake Aliyefahamika kwa Jina la Seif  Baada ya Kuipatia Timu ya Moroveteran Goli na nne

Timu ya Soka ya Moro Veteran ya Mkoani Morogoro Leo  Wameichapa Timu ya Golani Veteran ya Kimara Dar es Salaam jumla ya Magoli 4 kwa Moja.Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro Ulikuwa wa Kasi na Upinzani wa hali ya Juu.
Hadi Mapumziko Matokeo Yalikuwa Sare ya Bila Kufungana.
Kipindi cha Pili Moro Vetrani Walifungua Karamu ya Mgoli Katika Dk 50 Goli lilofungwa Na Seif baada ya Kupewa Pasi na Kufumua Shuti lilomshinda Golikipa.
Moro Veterani Waliendela Kulishambulia Goli la wapinzani Wao Na Kufanikiwa Kupata Mabao Mawili Katika Dakika za 67 na 70 Kupitia kwa Mshambulizi wao Khamis .
Magoli hayo yaliwachanganya Benchi la Ufundi la Gorani Veterani hali Iliyowafanya Kufanya Mabadiliko Haraka  na Kuwasaidia Kupata Bao La kufuta Machozi Katika Dk 79 ya Mchezo.Wakiwa Bado  wanaimani wanaweza Kuzudisha Magoli mawili yaliosalia walijisahau Na kukuta wakipigwa Goli na 4 katika Dk 87 Ya Mchezo Goli Lililofungwa na Khamisi Madole.
Hadi Mwisho Moro Veteran 4 Golani Veteran 1
Na MATUKIO NA VIJANA BLOG

No comments:

Post a Comment