Search This Blog

Thursday, February 13, 2014

MAHOJIANO NA KATIBU MKUU WA TFF KUHUSU SUALA LA OKWI - SOMA NA SIKILIZA ALICHOSEMA

Hivi punde mtandao huu umepata nafasi ya kufanya mazungumzo na Katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini Celestine Mwesiga ili kujua undani wa suala la FIFA kumuidhinisha mchezaji Emmanuel Okwi kuichezea klabu ya Dar Young Africans.

Katika mazungumzo hayo Mwesiga amesema kwamba ni kweli FIFA wamemruhusu Okwi kuendelea kucheza soka wakati wenyewe wakishughulikia madai ya vilabu vya Simba SC na Etoile Du Sahel.

"Kwanza ningependa kusema kwamba kazi ya FIFA kwenye hili suala ilikuwa sio kumruhusu mchezaji kuichezea au kutoichezea Yanga, hilo suala lipo chini ya shirikisho la soka nchini TFF.

"Kilichotokea ni kwamba kulikuwa na malalamiko ya klabu ya Simba SC, juu ya uhalali wa uhamisho wa mchezaji Emmanuel Okwi kutoka SC Villa kwenda Yanga na pili juu ya deni lao wanaloidai klabu ya Etoile Du Sahel. FIFA wameridhika na suala la uhamisho wa Okwi kwenda Yanga kwa maana ulifuata vigezo vyote na walipata ITC.
"Pia kuhusu suala la deni la Simba wanayoidai Etoile, FIFA imeeleza kwenye email yake kwamba suala lipo pale pale lakini halina uhusiano na suala la Okwi kusajiliwa Yanga. Sisi kama TFF tutaendelea kulifuatilia kiundani kuhakikisha Simba wanapata haki yao."

Alipoulizwa kama suala la uhamisho wa Okwi kwenda Yanga halina tatizo lolote, hivyo Okwi ataruhusiwa kuichezea Yanga, Mwesiga alisema: "Kilichobaki sasa ni masuala ya ndani ya shirikisho. Tutaangalia kama mchezaji husika amekidhi vigezo vya kuweza kushiriki kwenye michuano mbalimbali hapa nchini, ikiwa atakuwa amekidhi basi tutakuwa hatuna kipingamizi chochote."

10 comments:

  1. Hongera FIFA, TFF, Clouds fm kwa kukata mzizi wa fitna na kukiri kuwa Yanga ilifuata taratibu zote ktk kumsajiri Emmanuel Okwi kutoka Villa S.S., na kwamba ni RUKSA kuitumikia klabu yake mpya ya Dar Young Africans. Karibu saaaaana jembe letu. Ila kuna Mhe. mmoja wa upande wa pili uache kuizungumzia Yanga na kuudanganya umma eti hawajui taratibu za usajiri na kwa Okwi watashushwa daraja. Hivi Mhe wewe umesahau uliwahadaa nini Wanasimba juu ya Kelvin Yondan, Mbuyu Twitwe, Mrisho Ngassa na juzi tuu ukawahadaa tena kwenye media juu ya Emmanuel Okwi!!!! Kaaa kimya kwa mambo usiyiyajua. "No research no right to speek!!!"

    ReplyDelete
  2. Hata TP Mazembe walipokata rufaa FIFA kupinga uamuzi wa CAF wa kuwanyang'anya ushindi dhidi ya Simba mwaka 2011 walishinda rufaa yao lakini mashindano yalikuwa yamemalizika.Kilichotokea hapa nio baadhi ya viongozi wa TFF ambao bado wana ushabiki wa kijinga walitaka kumhujumu Okwi na Yanga kwa maslahi yao binafsi.Mmoja wao ni yule ambaye bila aibu siku ya mechi ya nani mtani jembe alivaa fulana ya simba ikiwa na maandishi ya kumkejeli Okwi na kumsifia Mafisango huku akisahau kwamba sasa hivi yeye ni kiongozi mkubwa wa TFF NA USHABIKI ANAPASWA KUBAKIA NAO MOYONI..Huyu ni kiongozi wa TFF anayeitwa Nyange"Kaburu"

    ReplyDelete
  3. Hapa imeonyesha uzaifu mkubwa katika kufuata sheria za kimataifa, mtu ana ICT unakataa kwa sababu aliwahi kuwa mchezaji wa timu fulani? Hivi sisi hatuna wanasheria au uelewa wetu mdogo? ni aibu kama Taifa, hili halikupaswa kabisa kutokea, sasa deni la Simba linawahusu nini Yanga? Simba badala ya kufuatilia deni wanafuatilia OKWI yuko wapi?

    ReplyDelete
  4. Hata kwa Kapombe tusubiri hayo hayo, Malizni anakuja kuua mpira ni full usanii

    ReplyDelete
  5. SHAFFIH UMEABIKA SANA NA ROHO YAKO MBAYA. ULIONESHA KUUMIA MNO BAADA YS OKWI KUSAJILIWA YANGA HADI UKASHINDWA KULINDA MAADILI YA KAZI YAKO. NIMEKUSIKIA KWENYE KIPINDI CHA SPORT UKIWA VERY EMOTIONAL. UNAJIDHALILISHA SANA WEWE. NENDA KAOMBE KAZI SIMBA.

    ReplyDelete
  6. Hao FIFA wahuni tu na TFF,kuelezea mambo ya usajili wa okwi hayawahusu bila kueleza kwanini walimruhusu miezi sita Vila na kama anaruhusiwa kuingia mkataba wa zaidi ya hiyo miezi sita na timu nyingine na status ya uhalali wake kama mchezaji wa etoile ukoje ni sehemu ya ubabaishaji mkubwa. Na pia kwanini FIFA ijibu kwa email badala ya barua rasmi. Pamoja na matatizo ya Rage nimegundua mengine yanakuzwa na ubabaishaji uliokubuhu ktk soka haishangazi walipotaka Ronaldo ashibde ballon odor wakasogeza deadline. Wahuni kabisa hao

    ReplyDelete
  7. Hii TFF na Kamati yake ya Hadhi na Maadili ya Wachezaji ni hovyo kabisa, naanza kumkumbuka Leodger Chila Tenga, Malinzi na wahaya wake watatumalizia haka kampira ketu alikokabakiza Tenga!

    ReplyDelete
  8. Hapa Rage anawazingua Simba tu.Tena wamtake awaambie alipewa shilingi ngapi na Esperance ya Tunisia mwaka 2011kwa ajili ya kuwakatia rufaa ili TP Mazembe waondolewe kwenye mashindano kwani documents zote walimpa yeye.NA MSHIKO JUU

    ReplyDelete
  9. Nakushauri ukaombe kazi Simba, achana na kazi Clouds FM utawafanya watu wakichukie kipindi cha sport extra, mbona alipochukuliwa na sport villa hukupiga kelele? Au kwanini hamkumfuata kumrudisha Simba mkamchukua Tambwe? Kimekuuma sana Okwi kusajiliwa Yanga! Na atacheza tu baki na roho mbaya yako, unataka Okwi asicheze afanye kazi gani? Hata Maximo alipotaka kuja yanga ilikuuma sana ukafanya fitna, haya endelea kuota Okwi kurudi kuchezea Simba.

    ReplyDelete
  10. Nakushauri ukaombe kazi Simba, hapo Clouds hapakufai utawafanya watu wakichukie kipindi cha sport Extra! Kimekuuma sana Okwi kuchezea Yanga, ndiyo maana uliota Okwi kurudi Simba, kama kilivyokuuma Yanga walipokuwa wanafanya mazungumzo na Maximo, mbona hamkumfuata Okwi alipoanza kucheza Sports Villa? Unataka asicheze afanye nini? Auze maandazi? Acha roho mbaya omba kazi Simba tujue moja ndiyo maana walikutoa kugombea ujumbe TFF.

    ReplyDelete