Search This Blog

Thursday, February 6, 2014

LIVERPOOL VS ARSENAL: LUIS SUAREZ NA REKODI MBOVU YA UFUNGAJI DHIDI YA TIMU ZA TOP 4 - WIKIENDI KUIENDELEZA AU ATAIADHIBU GUNNERS?

Kiwango cha Luis Suarez msimu kimekuwa katika hali ya juu mno, waandishi kibao wa habari wamekuwa wakiandika makala za kumsifia huku thamani yake katika soko la usajili ikipanda maradufu. 
Lakini pamoja na kuwa rekodi nzuri za upachikaji wa mabao msimu huu - ila kuna kuna sehemu mshambuliaji huyu wa Uruguay anapata zero - hii namba ya mabao aliyoyafunga dhidi ya vilabu vikubwa kabisa vya ligi kuu ya England. 

Katika mabao yote 23 aliyoyafunga msimu huu, hakuna hata moja kati ya hayo lilotinga katika nyavu za vilabu vya Manchester United, Manchester City, Chelsea au Arsenal – vilabu vilivyoshika nafasi nne za juu msimu uliopita.

Kiundani zaidi, kati ya mabao hayo ni manne tu amezifunga timu 10 za juu katika msimamo wa ligi.

Je Suarez anavionea vilabu dhaifu tu? Hata ukiangalia rekodi za 

REKODI YA UFUNGAJI YA SUAREZ

Timu ambazo Suarez amezifunga msimu huu...
Sunderland (14th kwenye ligi)  mabao 2
Crystal Palace (17th) bao 1
West Brom (16th) mabao 3
Fulham (20th) mabao 2
Everton (5th) mabao 2
Norwich (15th)mabao 4
West Ham (18th)mabao 2
Tottenham (6th) mabao 2
Cardiff (19th) mabao2
Hull (13th) bao 1
Stoke (11th)mabao 2

REKODI DHIDI YA TOP 4
(Man Utd, Man City, Chelsea, Arsenal)
2013-14 – 23 goals, 0 against top four. (MECHI 4).
2012-13 – 30 goals, 4 against top four. (Mechi 8).
2011-12 – 17 goals, 2 against top four. (Mechi 8).
2010-11 – 4 goals, 0 against top four. (Mechi 3).
nyuma ya msimu huu, takwimu zinaonyesha hivyo. 
Ni mara 74 mshambuliaji huyo wa Uruguay ameweza kubusu mishipa ya kiganja chake akishangilia mabao anayoyafunga tangu ajiunge na Liverpool, lakini mabao 6 tu kati ya hayo amezifunga timu za TOP 4, na hayo yamepatikana baada ya mechi 23.

Wakati huo huo, amefunga mabao 11 dhidi ya timu ya Norwich. Pia katika miaka yote hii ameifunga Manchester United goli moja tu miaka miwili iliyopita katika dimba la Old Trafford.

Msimu huu, Suarez alifunga mabao 10 katika mechi nne tu mapema mwezi Desemba kabla ya Liverpool haijangia katika wakati muafaka wa kuamua hatma yao ya ubingwa msimu huu waliposafiri kwenda kucheza na Manchester City na Chelsea, katika michezo hiyo muhimu, Suarez alitoka kapa, huku Liverpool akifungwa mechi zote - pia alishindwa kufanya chochote katika mchezo dhidi ya Arsenal na hata dhidi ya Manchester United katika kombe la ligi - pia mechi hizo zote Liverpool walifungwa. 

Jumamosi hii, wanakutana na viongozi wa ligi Arsenal katika dimba la Anfield. Ndio kwa ukali wa Suarez kuzifumania nyavu dhidi ya timu za chini umeipa nafasi Liverpool ya kuweza kusogolea Top 3.
Ingawa kwa hilo ili liweze kutokea inabidi Liverpool ianze kushinda dhidi ya vilabu hivyo vikubwa, mabao na uchezaji mzuri wa Suarez unahitajika kufanikisha hilo.

Wapinzani wao wa Jumamosi, Arsenal, ndio timu ile ile iliyojaribu kumnyakua Suarez kutoka Merseyside kwenda London ya kaskazini wakati kiangazi walipotuma ofa ya £40m-plus-£1. 
Kwa kuwa na Suarez, iliaminika wangeweza kushindania ubingwa, lakini hata baada ya kumkosa wanaonekana kuwa vizuri mno katika harakati zao za kumaliza ukame wa miaka 9 bila kombe.  

Arsenal nao, wameshindwa kufnya vizuri dhidi ya kubwa kama United, City na Chelsea, kama ilivyo kwa Suarez.

Wikiendi hii Suarez ana nafasi ya kuwafunga midomo wachambuzi wa soka walio na mashaka juu ya uwezo wake dhidi ya vilabu vikubwa na kuiwezesha timu yake kuisogelea top 3 ya EPL. Je ataweza kuisimamisha Arsenal iliyo on fire???? Muda utatoa majibu. 



5 comments:

  1. Mathematical analysis! not right for football. Ni analysis inayofanywa kutaka kuonyesha kuwa Suarez ni striker wa kawaida tu. Otherwise angalia shuguli yake na timu hizo za juu ndani ya dak 90 hata kama hakufunga! Suarez ni bonge la striker, ana kila kitu kinachomfanya mchezaji kuwa bora. Asante.

    ReplyDelete
  2. Picha uliyoiweka pekee inaonyesha namna anavyokabwa na wachezaji wa timu hizo kubwa! Muulize Compay atakwambia kuhusu huyo jamaa!

    ReplyDelete
  3. MUANDISHI KUMBUKA KUWA SUAREZ HAJACHEZA MECHI NA MAN U MSIMU HUU USIHESABU MECHI 4 SEMA MECHI 3.

    ReplyDelete
  4. Turejeshe na misimu ya nyuma ndo utoe tathmini yako tofauti na hapo mwandishi unaramba ziro, mcmu huu wenyewe mechi km ya chelsea na ile ya Man city Liver walipotezwa na waamuzi kutokana na rafu za ajabu alizokuwa akifanyiwa, kuhusu game ya Arsenal Liver walielemewa pale Emirates ila Sureboy alikabwa mno, kuhusu top 4 kwa vile Liver nayo imo na hawezi kuifunga timu yake mwenyewe weka kuwa kashindwa kuzifunga timu zlizoko top 3 katka raundi ya kwanza. Asante sana

    ReplyDelete
  5. Suarezi alicheza dhidi Ya Man utd msimu huu Capital one na liver walitolewa na manutd

    ReplyDelete