Search This Blog

Friday, February 21, 2014

KIUFUNDI ZAIDI: KWANINI MOYES HAPATI MATUNDA MAZURI KUTOKA KWA JUAN MATA KATIKA MFUMO WA 4-4-2?


David Moyes alimsaini Juan Mata kutoka akiwa na matumaini na mategemeo makubwa. Juan Mata alionekana kama mtu atakayekuja kuleta mageuzi ya kuisadia timu hiyo kuingia hata kwenye Top 4. Hata hivyo hali imekuwa tofauti na matarajio, Manchester United ikishinda mchezo mmoja tu kati ya minne Mata aliyocheza. Moja ya vitu vinavyoachangia matatizo haya ni mbinu za kiufundi, hivyo je inafaa kwa Moyes kuangalia upya mbinu zake ili kupata matokeo mazuri kutoka kwa mchezaji wake wa gharama zaidi - Juan Mata?

Mahala aambapo amekuwa akichezeshwa Mata. 
Baadhi ya watu walihisi Moyes angebadili mfumo kwenda kutumia 4-2-3-1 ili kuweza kupata matokeo mazuri kutoka kwa Wayne Rooney, Mata na Adnan Januzaj nyuma ya mshambuliaji wa mbele Robin van Persie, ingawa hilo halijawezekana mpaka sasa. Mata amekuwa akichezeshwa kama kiungo wa kulia au kushoto. Dhidi ya Arsenal alichezeshwa kama kiungo wa kushoto, ingawa alijaribu kuingia ndani ili kuwa karibu na washambuliaji wawili wa mbele 
matttt

Kama mchoro wa picha unavyoonesha hapo juu, United walikuwa wanacheza na Arsenal inayogombea ubingwa ugenini, lakini hapo juu tunaona Mata alitumia muda mwingi katika maeneo ya ulinzi, akikaa sana nyuma katika eneo la kulinda zaidi lango la timu yake (kutokea kushoto pia). Huu mfumo kwa hakika huwezi kukupa matunda mazuri kutoka Mata ambaye anakuwa bora zaidi anapokuwa na mpira miguuni mwake. Ndio maana haishangazi kuona Mata hakuwa na mchezo mzuri siku hiyo, akitengeneza nafasi mbili tu kwa Van Persie.

Dhidi ya Fulham alicheza vizuri kiasi na kuwa na mpira muda mwingi, ingawa alifanya hivi akicheza kwenye winga ya kulia katika mchezo ambao ulitawaliwa na krosi kutoka kwa wachezaji wa kikosi cha Moyes. Man United ilijaribu kupiga krosi 82, staili ambayo sio tu imepitwa na wakati lakini pia ni staili ambayo ndani yake huwezi kuona ubora wa Juan Mata, ambaye hufanya vizuri kazi yake anapocheza katikati ya mistari ya safu ya ulinzi na kiungo, na sio pembeni.

Mahala kwa kubadilisha
Mata hakufanya vibaya dhidi ya Fulham, alitengeneza nafasi tano za kufunga kwa wachezaji wenzie na katika mechi nne alizocheza ametengeneza jumla ya nafasi 13 (namba ya nafasi alizotengeneza Ashley Young msimu mzima). Lakini angeweza kufanya vizuri zaidi. Dhidi ya Fulham alikuwa na mpira kwa muda mwingi na alikamilisha 96% ya pasi zake zote.
mattttaaaa

Lakini tatizo pekee la hizo pasi zilikuwa katika maeneo ya pembeni, hasa upande wa kulia. Haya sio maeneo ya kupata ubora wa Mata. Mata anahitaji kuchezeshwa kati kati ya safu ya ulinzi ya wapinzania na kiungo, mahala ambapo anaweza kutumia jicho lake la pasi nzuri kwenda kwa washambuliaji. Kama tunavyoona kwenye picha hapo juu, hakuwa na mamalka ya mchezo kwenye eneo hilo.

Wazo la kwanza mbadala na kumuondoa mshambuliaji mmoja na kumchezesha Mata namba 10, jambo litakalomfanya awe na mpira muda mrefu na kuutumia katika maeneo ambayo anataka, sio kurudi nyuma kama ambavyo alivyokuwa akifanya dhidi ya Arsenal. Alicheza kwenye eneo hili katika mchezo pekee wa ushindi wa United katika mechi nne zilizopita - mechi dhdi ya Cardiff, ambapo alitengeneza nafasi nne.

Moyes anaonekana hataki au anasita kuwatumia Januzaj, Mata na Rooney katika kikosi kimoja na Van Persie. Hii inawezakana inatokana kwamba wachezaji wake wote watatu wa zamani wana uwezo wa kuingia ndani nyuma ya mshambuliaji wa kati. Njia pekee ya kufanya mfumo huu kufanya kazi ni kuachana na mfumo wa krosi na kuachia mpira wa pasi zaidi kuelekea ndani utumike zaidi.

Hitimisho
Hivi sasa David Moyes hapati matunda bora ya Juan Mata. Mfumo wa kutumia krosi ambayo Mata anatumika katika winga sio mzuri katika kutaka kupata matunda ya Juan Mata. Mata anahitaji uhuru wa kufanya kazi yake katika maeneo yake ya kati ya uwanja, hasa kwenye eneo la nyuma ya mshambuliaji. Ikiwa Moyes atabadili mfumo kwenda 4-2-3-1 ambao unamfiti Mata, Januzaj na Rooney wakicheza nyuma ya Van Persie. Jambo pekee la kuzingatia ni kuhakikisha mabeki wa pembeni wanakuwa na uwezo wa kutoa msaada mkubwa wakati timu inaposhambuliwa. Moyes hana cha kupoteza hivi sasa - hasa baada ya mfumo wa sasa wa 4-4-2 kutokuwa na matunda kwa timu na kupelekea matokeo mabaya. 

No comments:

Post a Comment