Search This Blog

Sunday, January 19, 2014

YUSUF MANJI AMPIGA MARUFUKU MZEE AKILIMALI KUZUNGUMZIA MAMBO YA KLABU,WANACHAMA WAUNGA MKONO.

MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yusuph Manji, aliibua cheleko ndani ya Mkutano wa klabu hiyo, baada ya kumtaka Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa klabu hiyo Ibrahim Akilimali kuacha kuzungumza ovyo ovyo katika vyombo vya habari wakati Katiba ya klabu yao haimpi mamlaka. Manji aliyasema hayo, katika Mkutano wa mwaka wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam, baada ya kujibu swali la mwanachama Msham Wazir ambaye ni Mwenyekiti wa Tawi la Bunju lilohoji kuwa, Wanachama hawatambui nani ni nanni ndani ya klabu kwa kuwa kila mtu anajifanya msemaji huku akimtolea mfano Akilimali.


Baada ya swali hilo, wanachama waliofurika katika ukumbi huo, walisimama na kushangilia na kumfanya Makamu Mwenyekiti Clement Sanga aliyekuwa akiongoza Mkutano huo kukabidhi rungu hilo kwa Manji baada ya yeye kutoa ufafanuzi kuwa, Katiba ya Yanga hakuna kifungu kinachowapa mamlaka wazee kuzungumza.
“Katiba ya Yanga haiwatambui wazee kabisa, na mtu akinielewa vibaya sawa tu, kwani hakuna sehemu ya katiba inazungumzia wazee, kwani Msemaji Mkuu katika klabu ya Yanga ni Mwenyekiti, Ofisa habari na hata mimi nazungumza endapo Mwenyekiti akiwa hayupo au ameniagiza,”alisema Sanga.



Aidha baada ya Sanga kujibu hivyo, alimkabidhi Manji jukumu la kufafanua suala hilo na kusema kuwa, Akilimali ni Mzee wake lakini anakuwa mvunjifu wa katiba ya Yanga kwa kusema sema katika vyombo vya habari mambo ambayo hayastaili kuzungumzwa.
“Akilimali anaongea kupita kiasi katika vyombo vya habari, kwani wewe sio msemaji wa klabu jamani, unavunja katiba ya Yanga, mambo ya nyumbani unaongea tu, eti Kaseja kafanyaje, jamani acha kufanya hivyo,”alisema Manji huku akiwaomba ridhaa wanachama waamue nini cha kumfanya Akilimali na kuwafanya wanachama kushangilia mwanzo mwisho.



Baada ya kusema hayo, Manji alinyanyuka katika kiti alichokuwa amekaa na kumfuata Akilimali na kuanza kuzungumza naye, huku wanachama wakishangilia na wengine kuzomea kitendo hicho.
Akizungumzia sakata hilo, Akilimali alikiri kukiuka katiba ya Yanga, na kusema kuwa, anahisi alipandwa na wazimu bila kujijua na ndio sababu ya kuongea katika vyombo vya habari bila idhini ya uongozi wake.
“Mimi kusema kweli sina kinyongo kabisa, na uongozi wangu, wamenizuia nisiongee katika vyombo vya habari, basi nitafanya hivyo, naisi ni wazimu tu na ushabiki ulinipanda, nawaheshimu na kuwasikiliza viongozi wangu, kama wamenipa onyo sawa tu,”alisema.

4 comments:

  1. Huyu mzee ni kilaza sana! Anashndwa kutambua kwamba UZEE NI BUSARA,MVI NI RANGI YA NYWELE TU!!

    ReplyDelete
  2. Kweli mzee anachonga sana kama kasuku bwana

    ReplyDelete
  3. Ama Kweli maskini akui,mzee mzima anapelekeshwa na mwenyekiti kisa uwezo wa kifedha...hili tatizo

    ReplyDelete
  4. No sio uwezo wa kifedha ni uwezo wa Katiba ya yanga ambayo akilimali.na wanachama wote wa yanga wameapa kuilinda na kuiheshimu.Katiba ina uwezo sana ndio mana unaona hata simba pale Rage anawapelekesha kwa kutumia uwezo ilionao Katiba ambayo yeye kama mwenyekiti ndio msimamizi mkuu wa hiyo Katiba.Nilitaka kuliweka sawa hilo tu-Katiba ndio mama.

    ReplyDelete