Search This Blog

Wednesday, January 8, 2014

YANGA YATOA MILIONI 10 KWA WARATIBU WA KOMBE LA MAPINDUZI.


Uongozi wa klabu ya Dar es salaam Young Africans leo umepiga hodi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa kina kwa waratibu wa michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuamua kujitoa dakika za mwisho kabla ya mashindano hayo kuanza.

Clement Sanga makamu mwenyekiti wa Yanga amethibitisha hilo ikiwa ni pamoja na klabu ya Yanga kutoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa kamati hiyo ya maandalizi,pia Yanga imetoa ahadi ya kwenda visiwani humo kucheza michezo ya kirafiki na pesa zote zitakazopatikana kutokana na viingilio zitakwenda kwenye mfuko wa maandamalizi wa Kombe la Mapinduzi.

BOFYA HAPA CHINI KUMSIKILIZA SANGA.

No comments:

Post a Comment